24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

KIONGOZI WA WALINZI CUF AFUKUZWA

Na Muhammed Khamis (UoI)-Zanzibar


cufCHAMA cha Wananchi (CUF) tawi la Kidatu C  Jimbo la Mtoni Unguja, limemfukuza uanachama aliyekuwa kiongozi wa walinzi wa chama hicho, Thiney Juma Mohamed kwa madai ya utovu wa nidhamu.

Akizungumza na gazeti hili jana, Mwenyekiti wa tawi hilo, Ali Abdalla Khatib alisema kabla ya kufikia uamuzi huo, waliitisha mkutano mkuu wa wajumbe wote ambao ulimjadili kwa kina juu ya tuhuma zilizokuwa zikimkabili.

Alisema mkutano huo, ulimjadili  Mohamed kutokana na taarifa yake aliyoitoa kwenye vyombo vya  habari kupinga namna  utaratibu wa uendeshaji wa chama unavyofanywa, huku akihusisha baadhi ya viongozi wakuu kuvunja Katiba.

“Hili ni kosa, chama chetu kina msemaji wake haiwezekani utoke na kusema kwenye vyombo vya habari wakati wasemaji wa chama wapo,’’alisema.

Alisema mkutano huo, ulimpa fursa Mohamed na alikiri kufanya hivyo, huku akiomba msamaha.

Akijibu tuhuma hizo, Mohamed alisema kitendo cha kuzungumza na vyombo  vya habari si kosa, kwa sababu alitoa maoni yake.

Kwa upande wake, Mkurugenzi wa Habari,Unenzi na Mahusiano ya Umma, Salim Biman alisema chama hicho ni taasisi iliyo imara inayohitaji kuendeshwa kama zilivyo taasisi nyingine.

“Kilichofanywa na tawi la Kidatu C, ni sawa maana wamemwona mwanachama wao ana hatia na ndiyo maana wameamua kumfukuza,”alisema Bimani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles