25.7 C
Dar es Salaam
Friday, April 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi wa upinzani Zimbabwe apigwa faini kwa kujitangazia ushindi

HARARE, ZIMBABWE

MAHAKAMA ya Zimbabwe jana ilimtia hatiani kiongozi maarufu wa upinzani, Tendai Biti kwa uhalifu wa uchaguzi na kumpiga faini kwa kujitangazia ushindi katika matokeo ya urais.

Biti, waziri wa zamani wa fedha aliyekuwa akiheshimika, alikitangazia chama chake cha Movement for Democratic Change (MDC) ushindi katika Uchaguzi Mkuu wa Julai 30, 2019, ambao ulishuhudia maandamano dhidi ya Serikali ambayo yalizimwa na jeshi. Watu sita waliuawa katika machafuko hayo.

Hakimu Gloria Takundwa aliamuru Biti alipe faini ya dola 200 (zaidi ya Sh 423,000 za Tanzania) au aende jela kwa wiki moja.

Pia alipewa adhabu ya kifungo cha miezi sita jela ambacho kilisimamishwa kwa miaka mitano.

Kiongozi wa MDC, Nelson Chamisa, ambaye alikuwa mahakamani, alisema kutiwa hatiani huko kunatia doa kubwa katika siasa za nchi.

Zimbabwe ilijikuta katika machafuko kufuatia uchaguzi huo wa kwanza katika historia ya nchi bila kuwapo Rais wa zamani, Robert Mugabe aliyejiuzulu baada ya jeshi kuingilia kati Novemba 2017.

Rais Emmerson Mnangagwa alikuwa ameahidi kutorudia kwa siasa za vitisho, wizi wa kura zilizoshuhudiwa wakati wa Mugabe, lakini ucheleweshaji matokeo uliwakasirisha wapinzani na kusababisha maandamano.

Mnangagwa, mrithi wa Mugabe katika kukiongoza Chama tawala cha ZANU-PF, alitangazwa mshindi lakini MDC ilikataa.

Biti alikimbia nchi kwenda Zambia wakati wa kilele cha machafuko lakini akarudishwa Zimbabwe licha ya kuomba hifadhi ya kisiasa na kusababisha kelele duniani.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles