25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

KIONGOZI WA UPINZANI URUSI AKAMATWA

MOSCOW, URUSI


KIONGOZI Mkuu wa upinzani nchini Urusi Alexei Navanly, amekamatwa wakati wa maandamano ya kupinga ufisadi aliyoandaa kwenye mji mkuu Moscow.

Navalny ni maarufu kwa kampeni zake za kupinga ufisadi, ambazo huwalenga maafisa wa vyeo vya juu walio karibu na Serikali ya Urusi.,

Amezuiwa kukabilana na Rais Vladimir Putin katika uchaguzi mkuu wa mwaka ujao, baada ya kupatikana na hatia katika kesi anayoitaja kuwa ilichochewa kwa misingi ya siasa.

Waandamanaji kadhaa walikamatwa, pale polisi walipojaribu kuvunja maandamano katika mji wa Vladivostok, kando ya Bahari ya Pacific.

Waandamanaji huko Chelyabinsk, walitaka Waziri Mkuu Dmitry Medvedev ajiuzulu kwa tuhuma za ufisadi.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles