28.9 C
Dar es Salaam
Friday, July 19, 2024

Contact us: [email protected]

Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akataa kuzindua bweni la wanafunzi

*TAKUKURU anachunguza ujenzi huo

Na Mwandishi Wetu, Singida

Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava amekataa kuweka jiwe la msingi katika bweni la wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani Mkalama baada ya kubaini kuwa ujenzi wa bweni hilo na uzio unachunguzwa na Taasisi ya Kuzui na Kupambana na Rushwa -Takukuru- wilaya ya Mkalama.

Kiongozi huyo wa Mbio za Mwenge wa uhuru amemwagiza Mkuu wa Takukuru wilaya ya Mkalama kumpatia taarifa ya awali ya uchunguzi hapo kesho ili waweze kujiridhisha kuhusu uchunguzi unaofanywa kwa sasa na Taasisi hiyo.

Ujenzi huo wa Bweni la Wanafunzi wenye Mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani Mkalama umegharimu zaidi ya Sh milioni 140.

Mnzava pia amewataka Watendaji wa Halmashauri ya Mkalama kumpatia taarifa kuhusu mchakato wa ukataji wa bima za afya kwa wanafunzi wenye mahitaji maalum kwenye shule ya msingi darajani ili kujua kama kwenye kama gharama za kuwakatia bima wanafunzi hao zimefuata taratibu.

Akiwa katika shule ya Sekondari ya Mkalama One, Kiongozi huyo wa mbio za mwenge wa Uhuru ametoa muda wa siku Saba kuanzia sasa kupatiwa taarifa kuhusu kwa nini ujenzi wa shule hiyo ya Sekondari ya Mkalama haujakamilika licha ya Serikali kutoa zaidi ya Sh milioni 544.

Amesisitiza kuwa nia ya Serikali ya kujenga shule za msingi na Sekondari nchini ni kusogeza huduma karibu na wananchi hivyo ni muhimu kwa Watendaji kusimamia miradi hiyo kikamilifu kulingana na thamani ya fedha na sio vinginevyo.

Awali akitoa taarifa kuhusu miradi ya maendeleo kwa Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa uhuru, Mkuu wa wilaya ya Iramba Moses Machari amesema mwenge huo wa uhuru utatembelea,kukagua, kuweka mawe ya msingi pamoja na kuzindua miradi ya maendeleo Saba yenye Thamani ya zaidi ya Sh bilioni Mbili.

Kitengo Cha Mwasiliano

Ofisi ya Mkuu wa mkoa wa Singida.

0755 516 591

0712762097

PTC 1. Godfrey Mnzava – Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru akizungumza wakati wa kutoa ujumbe wa Mbio za Mwenge wa Uhuru kwa wananchi wa wilaya ya Mkalama mkoani Singida.

PTC 2. Kiongozi wa Mbio za Mwenge wa Uhuru Godfrey Mnzava akimpatia kitambulisho cha bima ya Afya wanafunzi wenye mahitaji maalum katika shule ya msingi Darajani wilayani Mkalama.

PTC 3. Mwonekano wa Bweni la Wanafunzi wenye Mahitaji Maalum katika shule ya msingi Darajani ambalo Kiongozi wa mbio za Mwenge wa Uhuru amekataa kulizindua kutokana na Kuchunguzwa na Takukuru.

PTC 4– Makabidhiano ya Mwenge wa Uhuru kati ya Mkuu wa wilaya ya Iramba Suleiman Mwenda na Mkuu wa wilaya ya Mkalama Moses Machari.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles