26.9 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

KIONGOZI WA IRAN AIKOSOA SAUDI ARABIA

TEHRAN, IRAN


KIONGOZI wa kidini wa hapa, Ayatollah Ali Khamenei, ametoa matamshi makali dhidi ya hasimu wake Saudi Arabia.

Akihutubia waumini wa dini ya Kiislamu wakati wa kuanza kwa mwezi mtukufu wa Ramadhan, Ayatollah Khamenei ameishtumu Saudi kuwa ina uhalifu mwingi na haifuati misingi ya Korani.

Amesema kwamba viongozi wa Saudi, ‘ Ni kama wanakamuliwa kama Ng'ombe' na Marekani"

Saudia ilikubali kununua silaha zitakazogharimu zaidi ya dola bilioni moja kutoka Marekani, mpango ambao ulisainiwa rasmi wakati wa ziara ya Rais wa Marekani Donald Trump nchini humo wiki iliyopita..

Saudi Arabia ni mshirika mkuu wa Marekani katika juhudi za kukabiliana na ushawishi wa Iran eneo la Mashariki ya Kati.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles