28.3 C
Dar es Salaam
Saturday, November 26, 2022

Contact us: [email protected]

Kiongozi UVCCM apandishwa kizimbani

jpglengai-ole-sabayaNa JANETH MUSHI, ARUSHA

MWENYEKITI wa Jumuiya ya Umoja wa Vijana wa CCM (UVCCM) Mkoa wa Arusha,  Lengai ole Sabaya, amefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Arusha   akikabiliwa na mashitaka ya kujifanya mtumishi wa Idara ya Usalama wa Taifa (TISS).

Sabaya alifikishwa mahakamani hapo jana baada ya kukamatwa na polisi mwishoni mwa wiki.

Mbele ya Hakimu Mkazi wa mahakama hiyo, Gwantwa Mwankuga, Wakili wa Serikali, Lilian Mmasi, alidai   kosa la kwanza linalomkabili mtuhumiwa huyo ni kujifanya ofisa wa Idara ya Usalama wa Taifa.

Alidai   Mei 18 mwaka huu katika Hoteli ya Sky Way iliyopo makao mapya  Arusha, mtuhumiwa alijifanya mwajiriwa wa idara hiyo.

Wakili Mmasi alilitaja shitaka la pil kuwa ni la kughushi nyaraka ambako mtuhumiwa anadaiwa kughushi nyaraka za idara hiyo mwaka huu, katika siku isiyofahamika na kufanikiwa kupata kitambulisho cha idara hiyo chenye picha yake.

Kwa mujibu wa wakili huyo, kitambulisho hicho kilikuwa na maneno yaliyosomeka ‘Saturday. Code. Eagle 3 Idara ya Usalama wa Taifa chenye namba MT. 86117’

Sabaya alikana kutenda makosa hayo na Wakili Lilian aliiambia mahakama hiyo, kuwa upelelezi wa kesi hiyo haujakamilika.

Wakili   aliiomba  mahakama hiyo ipange tarehe nyingine ya kutaja kesi hiyo.

Wakili wa utetezi, Yoyo Asubuhi, aliiomba mahakama hiyo kumpa mteja wake dhamana  akisema  mashitaka aliyoshitakiwa nayo yana dhamana.

Hakimu Mwankuga alikubaliana na ombi hilo na kumtaka Sabaya kuwa na wadhamini wawili wanaoaminika na kila mdhamini awe na hati ya dhamana ya Sh milioni tatu.

Shauri hilo liliahirishwa hadi Oktoba 5 mwaka huu litakapotajwa tena.

NJE YA MAHAKAMA

Akizungumza na waandishi wa habari nje ya mahakama, Sabaya alisema amepata heshima kubwa kufikishwa mahakamani kwa kuwa wabaya wake wataumbuka.

“Waliopika majungu dhidi yangu kwa dakika 45 nje ya mahakama, wajue dakika 45 zilizosalia zitachezwa ndani ya mahakama na haki yangu itapatikana,” alisema Sabaya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,558FollowersFollow
557,000SubscribersSubscribe

Latest Articles