28.2 C
Dar es Salaam
Sunday, December 1, 2024

Contact us: [email protected]

KINYWAJI CHA K-VANT KUPATIKANA KATIKA CHUPA MPYA

Na MWANDISHI WETU

-DAR ES SALAAM

KAMPUNI ya Mega Beverage Company Limited ya mkoani Arusha, inayotengeneza pombe kali chapa maarufu ya K Vant, imezindua chupa mpya za kinywaji cha K-Vant zenye mwonekano tofauti na chupa za awali.

Mabadiliko hayo hayakubadilisha ladha halisi ya kinywaji hicho na wateja wake wataendelea kuifurahia ikiwa katika ladha yake halisi ya siku zote.

Hafla ya uzinduzi huo ilifanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam, ambapo mgeni rasmi alikuwa ni Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Walemavu, Antony Mavunde.

Akizungumza kwenye hafla hiyo ya uzinduzi, Mavunde alipongeza  hatua ya kampuni hiyo kubuni mkakati wa kuongea soko la bidhaa na kuongeza kuwa masoko yakiongezeka ndivyo mapato ya serikali yanaongezeka kupitia kulipa kodi sambamba na kuongeza wigo wa  ajira kutokana na kuhitajika nguvu kazi zaidi.

“Serikali ya awamu ya tano ina mkakati wa kuifanya Tanzania nchi ya viwanda, tutazidi kuboresha mazingira zaidi kwa wawekezaji katika sekta hii ili lengo la kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta hii lifanikiwe haraka  sambamba na kupunguza changamoto ya tatizo la ajira kwa vijana,” alisema Mavunde.

Awalia akitoa taarifa kwa Mkurugenzi wa Masoko wa Mega Beverage Company Limited, Marco Maduhu, alisema: “Kauli mbiu yetu ya kinywaji cha K-Vant katika mwonekano mpya ni ‘Ni Halali Yako’ .  Kampuni imejipanga  kuimarisha usambazaji wa bidhaa ya pombe ya K-Vant katika sehemu zote nchini ili Watanzania waendelee kufurahia ubora wake kikiwa katika mwonekano wa chupa mpya na katika ladha ileile waliyoizoe kuipata siku zote,” alisema.

Alisema uzinduzi wa chupa mpya za K-Vant mbali na kufanyika katika Mkoa wa Dar es Salaam, pia utafanyika katika mikoa ya Arusha na Mwanza, pia usambazaji wa kinywaji hiki kwenye mwonekano mpya katika ladha yake halisi utaendelea kufanyika katika mikoa yote nchini  kuanzia sasa.

“Wateja wetu wowote popote mlipo tunawashukuru kwa kuendelea kutuunga mkono, nasi tutaendelea kuboresha huduma zetu za usambazaji na kuhakikisha kinywaji bora cha K-Vant kinawafikia popote mlipo kikiwa katika chupa mpya,” alisisitiza.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles