30.2 C
Dar es Salaam
Saturday, April 1, 2023

Contact us: [email protected]

Kinondoni yatumia milioni 500/- kukabili kipindupindu

DSC_0092NA NORA DAMIAN, DAR ES SALAAM

HALMASHAURI ya Manispaa ya Kinondoni imetumia zaidi ya Sh milioni 500 kupambana na   kipindupindu tangu kilipozuka Agosti 15 mwaka huu.

Hadi sasa watu 1194 wameugua ugonjwa huo katika Manispaa hiyo na 17 wamefariki dunia.

Akizungumza   baada ya kupokea msaada wa dawa na vifaa tiba uliotolewa na Benki ya CRDB, Mkurugenzi wa Manispaa hiyo,   Mussa Natty, alisema kila siku kuna wagonjwa wapya wanaripotiwa na jana walikuwa 15.

Msaada huo wenye thamani ya Sh milioni 15 ulitolewa na benki hiyo kupitia sera yao ya kurudisha faida kwa jamii katika Wiki Maalum ya Huduma kwa Wateja inayoadhimishwa na benki hiyo kila mwaka.

“Ni gharama kubwa sana kumuhudumia mgonjwa wa kipindupindu, katika kila nyumba anayotoka mgonjwa lazima tumwage dawa nyumba 10 zinazomzunguka, tumetoa sana elimu lakini hali bado si nzuri na kesho (leo) tutakutana na wenyeviti wote kuangalia namna ya kudhibiti ugonjwa huu,” alisema Natty.

Naye Mkurugenzi Mtendaji wa CRDB, Dk. Charles Kimei, alisema Wiki Maalum ya Huduma kwa Wateja itaadhimishwa Oktoba 5 hadi 11 mwaka huu katika matawi yote ya benki hiyo   Tanzania Bara na Visiwani.

Naye Herieth Faustine anaripoti kuwa  katika Manispaa ya Temeke   wameripoti wagonjwa 211  huku Ilala kukiwa na wagonjwa 968, hali iliyosababisha manispaa hizo kupiga marufuku uuzwaji wa vyakula holela ikiwa ni jitihada za kupambana na ugonjwa huo.

Ofisa Habari wa Manispaa ya Ilala, David Langa alisema  jana kuwa idadi hiyo imekuwa ikiongezeka na   kwa jana walipokelewa wagonjwa 28 kutoka katika kaya tofauti  ndani ya manispaa hiyo.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
211,391FollowersFollow
564,000SubscribersSubscribe

Latest Articles