25.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, April 23, 2024

Contact us: [email protected]

Kinondoni Mabingwa Pool “88” Kitaifa

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

TIMU ya Pooltable ya Snipers yenye makazi yake Mwenge Mpakani ya Mkoa wa Kimichezo wa Kinondoni wameibuka Mabingwa katika fainali za Kitaifa za Mashindano ya Pooltable yajulikanayo kama “88” National Pool Competitions 2022 yaliyomalizika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa wa ndani(Benjamin Indoor Stadium).

Baadhi ya Wachezaji na mashabiki wa timu ya Snipers ya Kinondoni wakishangilia mara baada kuibuka mabingwa wa fainali za kitaifa za mchezo wa Pooltable kwa kuwafunga timu ya Fuoni ya Zanzibar 13 – 7, zijulikanazo kama “88 National Pool Competitions 2022” zilizomalizika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Taifa wa Ndani jijini Dar es Salaam.

Snipers walitwaa ubingwa huo kwakuifunga timu ya Fuoni kutoka Zanzibar 13 – 7 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Sh milioni moja(1,000 000). Timu ya Fuoni pamoja na kufungwa ilichukua nafasi ya pili na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Sh laki nne(400,000).

Wakizungumza kwa nyakati tofauti Wakurugenzi wa timu mbili hizo akianza Mkurugenzi wa Snipers kutoka Kinondoni kwanza alishukuru waandaaji wa mashindano hayo na washiriki wote kutoka mikoa yote lakini pia aliwapongeza timu ya Fuoni kwa ushindani ambao ulikuwa mzuri lakini mwisho wa siku timu ya Snipers wameibuka mabingwa na kuwaomba wakajipange mwaka ujao.

Nae Mkurugenzi wa Fuoni ya Zanzibar, Vishen Bhaiya alishukuru kwa maandalizi mazuri ya mchezo pamoja na mpangilio wote kwa ujumla lakini pia aliwapongeza Snipers kwa mchezo mzuri wa ushindani na kuahidi mwakani atajipanga vizuri ili achukue ubingwa huo.

Upande wa mchezaji mmoja mmoja(singles) Wanaume, Baraka Jackson kutoka Manyara aliibuka bingwa wa mashindano hayo kwa kumfunga Salim Yusuf Beano kutoka Zanzibar 11–7 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Sh laki tano(500,000).

Nafasi ya pili ya mashindano hayo ilichukuliwa na Salimu Yusuf Beano ambaye alizawadiwa pesa taslimu shilingi laki mbili na nusu(250,000).

Upande wa Wanawake mchezaji mmoja mmoja (Singles), Jackline Tido kutoka Dodoma alitwaa ubingwa kwa kumfunga Grace Shindika 7 – 2 na hivyo kuzawadiwa pesa taslimu Sh laki moja(100,000).

Mshindi wa pili Wanawake ni Grace Shindika ambaye alizawadia pesa taslimu shilingi elfu hamsini(50,000).

Akizungumza baada ya kukabidhi zawadi mratibu wa mashindano ya nane nane yajulikanayo kama “88 National Pool Competitions 2022, Michael Machela aliwashukuru timu zote zilizoshiliki mashindano hayo kuanzia ngazi za mikoa hadi Taifa.

Pia aliwapongeza wachezaji wote walioshiriki kwa upande wa timu pamoja mchezaji mmoja mmoja Wanaume kwa Wanawake.

Mwisho aliwapongeza Mabingwa Snipers kutoka Kinondoni, Bingwa wa mchezaji mmoja mmoja(Singles) Baraka Jackson kwa mara ya pili kutwaa ubingwa wa mashindano hayo na Jackline Tido kutoka Dododoma kwa upande wa wanawake.

Machela alimaliza kwa kutoa wito mwakani tujiandae vizuri kwa ushindani na si kushiriki kwani pia mwakani mikoa itaongezeka. Mikoa iliyoshiriki mashindano ya Taifa ni, Mbeya, Manyara, Morogoro, Ilala, Kinondoni na wenyeji Temeke.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles