31.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kingu: Mama ‘amewashika’ kupitia wizara ya January

Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital

Mbunge wa Singida Magharibi, Elibariki Kingu amesema Serikali ya Rais Dk. Samia Suluhu Hassan imefanya vizuri na kuwaziba midomo wapinzani kupitia Wizara ya Nishati inayoongozwa na January Makamba.

Kingu ameyasema hayo mapema leo Mei 31, wakati akichangia mjadala wa bajeti ya Wizara ya Nishati iliyowasilisha mapema leo na Waziri Makamba.

“Na kule wanakopita watu wa Chadema (Chama Kikuu cha Upinzani nchini) wanapiga propaganda kwamba rais anaweka mabango, nataka nikuambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia wizara yako January.

“Nataka niwaombe wabunge wote tuendelee kumuunga mkono Makamba na Mama Samia na wizara hii, tuendelee kuwashika mkono. Kazi wanayoifanya ni kubwa,” amesema Kingu na kuongeza kuwa:

“Sisi kwenye Ilani tuliwatuma mtuwashie umeme, umeme unawaka unataka nisikusifie?. Na kule wanakopita watu wa Chadema wanapiga propaganda kwamba rais anaweka mabango, nataka nikuambie ukiona mtu anapiga kelele jua umembana vizuri, Mama amewashika kwelikweli kupitia Wizara yako Makamba,” amesema Kingu.

Mapema leo Waziri Makamba aliwasilisha bungeni makadirio ya bajeti ya wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha wa 2023/24 akiomba kuidhinishiwa Sh Trilioni 3.04.

“Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu sasa liidhinishe Bajeti ya jumla ya Shilingi 3,048,632,519,000 kwa ajili ya matumizi ya Wizara ya Nishati na Taasisi zake,” amesema Makamba.

Kwa mujibu wa Waziri Makamba mchanganuo wa fedha hizo ni kama ifuatavyo:
“Shilingi 2,960,702,821,000 sawa na asilimia 97.1 ya Bajeti yote ya Wizara ni kwa ajili ya Miradi ya Maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 2,609,156,128,000 ni fedha za ndani na Shilingi 351,546,693,000 ni fedha za nje.

“Sh 87,929,698,000 sawa na asilimia 2.9 ni kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kati ya fedha hizo Sh 71,637,112,000 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo (OC) na Shi 16,292,586,000 kwa ajili ya Mishahara (PE) ya watumishi wa Wizara na Taasisi zilizo chini yake,” amesema Makamba.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles