Na Mwandishi Wetu Mtanzania Digital
MSANII wa muziki wa kizazi kipya kutoka nchini Nigeria, King Perry ameachia EP yake aliyoipa jina la Continental Playlist ikiwa na nyimbo saba, ikiwa ni miezi michache baada ya kuachia ngoma yake ya pili ya On God.
King Perryy aliyepata umaarufu mwaka 2018 baada ya kuachia ngoma yake ya Man On Duty aliyomshirikisha Timaya, amesema haikuwa kazi nyepesi kuikamilisha EP hiyo kwani alikuwa na ngoma zaidi ya 50 ambapo amefanya kazi kubwa ya kuchagua ni zipi ziingie kwenye EP hiyo.
Katika EP hiyo ya Continental Playlist ambayo nyimbo nyingi zipo katika mahadhi ya ‘dancehall’, King Perryy amewashirikisha mastaa wakubwa nchini Nigeria akiwemo
Tekno, Victony, Ria Sean na 1da Banton ambapo pia kuna nyimbo ambazo zipo kwenye mahadhi ya Afrobeats, reggae, pop na kadhalika.
Nyimbo zilizomo ndani ya albamu hiyo ni On God, Turkey Nla aliomshirikisha Tekno, Tight Condition aliomshirikisha Victony na Oh No.
Nyimbo nyingine ni Falling aliomshirikisha Ria Sean, No Stress na Denge ambao amemshirikisha 1da Banton.