31.2 C
Dar es Salaam
Friday, October 11, 2024

Contact us: [email protected]

KING  MASAKU TOKA 254 AWANASA RIYAMA ALLY, JB, RICH RICH

NA SWAGGAZ RIPOTA

WAKATI  kukiwa na minong’ono ya soko la filamu nchini kuyumba kutokana na sababu kadha wa kadha, wageni kutoka nje wa Bongo tayari wameiona fursa na tayari wameanza kuzichangamkia.

Elisha Masaku maarufu nchini Kenya (254) kwa jina la King Masaku ni miongoni mwa wasanii walioiona fursa kwenye tasnia ya filamu nchini. Msaku amejaaliwa vipaji lukuki kwani ni mwimbaji wa Gospo na msanii wa filamu za vichekesho.

Akizungumza na Juma3tata alipotembelea ofisi za gazeti hili, King Masaku anasema tayari ameanza kufuata nyayo za marehemu baba yake, msanii mkongwe ambaye kwa sasa ni marehemu Mbuthia Elias Masaku aliyewahi kutamba kwenye michezo ya kuigiza maarufu Afrika Mashariki za Tausi na Vitimbi akiwa na waigizaji wengine kama Mzee Pawang, Mama Kayai na Mzee Ojwang.

“Baba yangu alifanya kazi kubwa Kenya na Afrika Mashariki lakini alikufa masikini, kwangu sitaki itokee hiyo ndiyo maana najaribu kutanua wigo wa kazi zangu katika nchi mbalimbali,” anasema King Masaku.

Katika tete ambayo wasanii wengi nchini wamekuwa wakiisema, King Masaku ameiona kama fursa na tayari ameingia nchini kuifanyia kazi fursa hiyo.

“Ni rahisi sana msanii wa Tanzania kufanya vizuri Kenya na vile vile ni rahisi pia kwa msanii wa Kenya kufanya kazi Bongo, nimeamua kuja hapa kufanya kazi ili watanzania wanielewe, waifurahie sanaa yangu, nyumbani kwetu tayari nina mashabiki, siwezi kutembea sokoni bila kujificha, watu lazima watajaa kuniangalia,” anasema Masaku.

Masaku Jr ni mchekeshaji ambaye nchini Kenya hufananishwa na Kigwendu, anapendwa na mashabiki ambao wanadhani ni Kingwendu Jjambo ambalo analifurahia sababu hata yeye anamkubali mchekeshaji huyo wa Tz.

Msanii huyo hivi sasa yupo Dar es salaam kwa ajili ya kutengeneza mipango ya kazi na waimbaji wa Injili na wasanii wa filamu, King Masaku anasema anampenda Riyama Ally.

“Tayari nimekutana na Riyama, amefurahi kuniona na mimi napenda sanaa yake na muda ukifika tunaweza kufanya kazi ambayo itanitambulisha mimi Tanzania na yeye atazidi kujizolea mashabiki Kenya,” anasema.

Hali kadharika King Masaku amekutana na mwigizaji nyota, Jacob Steven ‘JB’ na Single Mtambalike ‘Rich Rich’ ambao anasema wamefurahi kumuona nay eye ameitumia nafasi hiyo kujitangaza na kutengeneza mazingira ya kazi.

“Nimekutana na JB, Mungu akijaalia tunaweza kufanya kazi mwezi Novemba, Kenya ana mashabiki wengi naamini nikifanya naye kazi atazidi kuwa juu na mimi nitafanikisha lengo langu kuliteka soko la filamu Tanzania, pia nilikutana na Rich Rich ni mtu mzuri sana,” anasema.

Siyo hao tu, King Masaku anatamani kukutana na mastaa wengine wa Bongo kama vile Christopher Mwahangila (mwimbaji Gospo), Wastara Juma, Gabo na wengine wengi ili awape njia ya kutengeneza fedha nchini Kenya kwani wanakubalika sana.

“Sanaa ya Tanzania ina soko sana Kenya, natamani nikutane na watu hao ili niweze kuwapa mbinu ya kuingiza fedha kutokana na kazi zao kukubalika kule, siyo mastaa hata chipukizi wanaweza kunicheki WhatsApp kwa namba +254 704 068 698,  au Facebook kwa jina la Masaku Elisha na Intagram  natumia King Masaku ili tuweze kupeana elimu hii muhimu,” anasema Masaku.

 

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
590,000SubscribersSubscribe

Latest Articles