27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, July 24, 2024

Contact us: [email protected]

Kinara NMB CDF Trophy kuondoka na pikipiki

Na Winfrida Mtoi, Mtanzania Digital

Wachezaji zaidi ya 100 wa gofu kutoka ndani na nje ya nchi wanachuana vikali katika shindano la Mkuu wa Majeshi ‘NMB CDF Trophy 2023’, huku mshindi wa jumla akitarajiwa kuondoka na zawadi ya pikipiki.

Katika shindano hilo lililoanza leo Septemba 2, 2023 kwa wachezaji wa ridhaa linatarajia kufikia tamati kesho kwenye viwanja ya Klabu ya Gofu Lugalo, jijini Dar es Salaam.

Kabla ya shindano hilo la ridhaa, jana walianza kucheza wachezaji wa kulipwa ambapo Abdallah Yusuf kutoka Lugalo amefanikiwa kuibuka mshindi wa jumla akitetea taji lake.

Meneja Klabu ya Gofu Lugalo, amesema shindano hilo ni muendelezo wa sherehe za kuzaliwa kwa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania (JWTZ) na mgeni la rasmi atakayefunga ni Mkuu wa Majeshi, Generali Jacob Mkunda.

Kanali Mziray amesema mwaka huu ushindani umekuwa mkubwa zaidi hali inayoashiria kukua kwa mchezo huo na kuondoa ile dhana ya kuwa gofu inachezwa na matajiri.

Naye Meneja Muandamizi wa Wateja Binafsi wa benki ya NMB, George Mrema, ameeleza kuwa wamefurahishwa na ushirikiano wanaondelea kuupata tangu wameanza kudhamini shindano hilo.

‘Kwa kweli ushindani ni mkubwa, tumefurahi kuwepo hapa na tumekuja na timu yetu ya NMB, lengo ni kuhakikisha tunaibuka washindi mwaka huu tofauti na mwaka. Pamoja na kucheza pia tunatoa masuluhisho ya kifedha,” amesema Mrema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles