27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

KINA SAKAYA WAPINGA KUSHTAKIWA CUF

MBUNGE wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF)
Na Kulwa Mzee-Dar es Salaam

MBUNGE wa Kaliua, Magdalena Sakaya (CUF), Mbunge wa Mtwara Mjini, Maftah Nachuma (CUF) na wenzake sita wamepinga kushtakiwa na Bodi ya Wadhamini ya CUF kwa madai kwamba haina mamlaka ya kuwashtaki.

Waliomba  maombi hayo yatupwe. 

Hoja za kupinga kushtakiwa ziliwasilishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jana mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu, Wilbroard Mashauri na Wakili wao, Mashaka Ngole wakati kesi hiyo ilipokuwa ikitajwa.

Mashaka aliwasilisha majibu ya kiapo kinzani kilichoapwa na wajibu maombi wote wanane pamoja na pingamizi la awali dhidi ya maombi yaliyopo mahakamani.

Katika pingamizi, wajibu maombi wanadai maombi hayawezi kusikilizwa katika mahakama hiyo kwa sababu yanashughulikiwa katika maombi namba 23/2016 yaliyopo Mahakama Kuu.

Anadai mwombaji hana miguu ya kusimamia kufungua kesi dhidi ya wajibu maombi hivyo maombi hayo hayana msingi kwa kushindwa kubainisha jina la mwandishi wa masuala ya fedha kwa sababu hiyo wanaiomba mahakama kuyatupilia mbali maombi hayo.

Wakili wa Bodi ya Wadhamini ya CUF, Hashim Mziray aliomba apewe   siku 11 kujibu   hati kinzani iliyowasilishwa na wajibu maombi.

Alidai atawasilisha majibu hayo Machi 31 mwaka huu na Mahakama iliamuru kusikiliza pingamizi la awali Aprili 12 mwaka huu.

Wakili Mziray aliwasilisha maombi madogo kwa hati ya dharura,  akiomba mahakama iwazuie kwa muda wajibu maombi kujihusisha katika masuala ya uongozi na kufanya mikutano ya chama.

Maombi hayo yaliyowasilishwa kwa hati ya dharura ni dhidi ya wajibu maombi, Sakaya, Nachuma, Thomas Malima, Omar Masoud, Abdul Kambaya, Salama Masoud, Zainabu Mndolwa na Jaffari Mneke.

Wakili Mziray aliomba maombi hayo yasikilizwe kwa haraka kwa akidai wajibu maombi wanataka   kufanya mikutano ya chama hicho, wakati hawana uwezo wa kufanya hivyo.

Bodi hiyo ya wadhamini ya CUF ilifungua kesi hiyo mahakamani hapo siku moja baada ya Mwenyekiti wa chama hicho, Profesa Ibrahim Lipumba kutangaza kutengua nafasi tano za wakurugenzi wa chama hicho na kutangaza majina mapya.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles