Kina Membe, Nape njiapanda

0
1212

Na MWANDISHI WETU – DAR ES SALAAM

MSIMAMO wa Waziri wa zamani wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Benard Membe, kuhoji kosa lake ili amuombe radhi Rais Dk. John Magufuli kutokana na kudaiwa kumsema vibaya kupitia mazungumzo ya simu, ni wazi sasa unamweka njiapanda.

Msimamo huo wa Membe umekuja siku chache tangu Rais Magufuli atangaze kuwasamehe wabunge wawili wa CCM; January Makamba (Bumbuli) na William Ngeleja (Sengerema) baada ya kumwomba msamaha kutokana na kumsema kupitia mazungumzo ya simu.

Wanachama wengine wanaotajwa katika sakata hilo; makatibu wakuu wastaafu wa CCM, Abdulrahman Kinana na Yusuf Makamba na aliyepata kuwa Katibu wa Itikadi na Uenezi wa chama hicho, Nape Nnauye, hawajaweka wazi msimamo wao kuhusu kuomba radhi.

Wakati Membe ambaye alizungumza na gazeti hili akihoji sababu za yeye kuomba radhi na iwapo tumejiridhisha kama wapo waliofanya hivyo, kwa upande wake Makamba alisema hataki na hana maoni juu ya suala hilo.

“Eeeh bwana wee sina maoni,” alisema kwa kifupi Makamba.

MTANZANIA Jumapili liliwatafuta bila mafanikio Kinana na Nape.

Ingawa watu wa karibu na Nape walisema ni vigumu kubashiri iwapo mwanasiasa huyo kijana ataomba radhi.

Iwapo Kinana, Makamba, Membe na Nape hawataomba radhi kwa Rais Magufuli, huenda …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here