26.1 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Kimwanga kuanza na miundombinu

 FARAJA MASINDE– DAR ES SALAAM

MGOMBEA udiwani Kata ya Makurumla, Bakari Kimwanga (CCM), amesema iwapo atachaguliwa Oktoba 28, jambo la kwanza atakalolifanya ni kuimarisha miundombinu.

Kimwanga aliyasema hayo mwishoni mwa wiki wakati akiwaomba kura wananchi wa Kilimahewa, Magomeni, Dar es Salaam.

PICHA: IMAN MKETEMA

Alisema barabara za mitaa hiyo haziendani na hadhi inayohitajika pamoja na kwamba zinatengewa fungu kutoka halmashauri.

“Ukiangalia miundombinu ya barabara zetu ambazo ni lango muhimu la kkiuchumi barabra zake haziakisi maisha ya kawaida, leo barabara zake zote zimekufa, lakini leo sisi watu wa Mkaurumla tumebaki tukitolea macho barabra za wenzetu badala ya zetu.

“Lakini sisi CCM tunaowaomba mtuamini baada ya Oktoba 28, saa 12 jioni na matokeo yakatoka diwani akawa Kimwanga, kazi yetu yakwanza tunakuja kuifanya Kilimahewa kwa ajili ya kurekebisha miundombinu yetu.

 “Unapozungumza barabara kama kiungo kikuu muhimu cha mawasiliano baina ya mtembea kwa mguu na vyombo vya moto haiwezi kuchochea uchumi kwa hali ilivyo pale, hivyo ndiyo maana CCM tunaomba mtuamini kuwa ndani ya miaka mitano barabara hiyo itakuwa imejengwa kwa lami,”alisema Kimwanga.

PICHA: IMAN MKETEMA

Alisema mbali na barabara, iwapo atachaguliwa atasimamia uimarishaji wa vivuko kwenye mtaa huo wa kilimahewa ndani ya mwaka mmoja.

“Vivuko vingi kwenye mtaa huu vimekuwa na changamoto ikiwmao kile cha kwandoto, tunajua kuna makundi ya vijana, wanawale na walemavu ambao kwa pamoja wamekata tama.

“Hivyo kama tunavyojua kwa mujibu wa sheria ya bunge iliyopitishwa ambayo inazitaka halmashauri zote nchini kuhakikisha kuwa zinatenga asilimia kwa ajili ya makundi haya hivyo haya tunaenda kuyasimamia haya kwa dhati baada ya Oktoba 28.

 “Tunakwenda kukata mnyororo huu wa kutoa mikopo kwa upendeleo, huku wale walengwa wakiachwa, ukiacha hilo kuna fedha za TASAF ambazo zinatolewa kwa kazya maskini, lakini ukweli ni kwamba kaya zilizoingizwa huko hasikustahili, hivyo tukipata fursa baada ya Oktoba 28, hayo yatabaki historia,”alisem Kimwanga.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,734FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles