27.5 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kimbunga hatari kuikumba mikoa ya kusini

Na ANDREW MSECHU DAR NA FLORENCE SANAWA, MTWARA

MAMLAKA za Hali ya Hewa Tanzania na Msumbiji zimethibitisha kuwapo kimbunga kilichopewa jina la Kenneth, kinachotarajiwa kuyakumba maeneo ya pwani ya Kusini mwa Tanzania na Kaskazini mwa Msumbiji kati ya leo usiku na kesho.

  Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Mamlaka ya Hali ya Hewa nchini (TMA), Dk Pascal Wanita, alisema tayari mamlaka hiyo imethibitisha kuwa kimbunga hicho kimeonekana katika maeneo ya Bahari ya Hindi.

Alisema mifumo ya hewa inaonyesha kimbunga Keneth kilichopo eneo la kaskazini magharibi mwa Kisiwa cha Madagascar, kinaambatana na mvua kubwa na upepo mkali katika eneo hilo.

“Kimbunga hicho kinaendelea kutawala mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa  nchini, hivyo kusababisha ongezeko la mvua inayoambatana na ngurumo za radi na upepo mkali kadri kinavyokaribia maeneo ya ukanda wa pwani.

“Katika bahari ya Hindi kuna kimbunga cha tropoki kinachojulikana kwa jina la Kenneth ambacho kwa vipimo vya hali ya hewa inaitwa ‘tropical cyclone destruction potential scale (CPDS).

“Hiki kinatabiriwa kuwa chenye uwezo wa kusababisha maafa katika kiwango cha sita kati ya viwango 10 vya juu ambavyo vipo maximum level 10 ambazo zipo,” alisema Dk Wanita. 

Alisema pamoja na kukaribua katika pwani ya Tanzania na Msumbiji leo, taarifa ya jana ilionyesha kilikuwa karibu zaidi na visiwa vya Moroni kwa umbali wa kilometa 500.

Alisema mpaka jana mchana kimbunga hicho kilikuwa kilomita 450 kutoka pwani ya Mtwara na kina kasi ya kilomita 130 kwa saa.

“Kufikia usiku wa leo (jana) Aprili 24 kimbunga hicho kitakuwa kilomita 250 kutoka pwani ya Mtwara, kikiwa kinasafiri kwa kilomita 150 kwa saa. Kimbunga hicho kinatarajiwa kuongeza nguvu zaidi Alhamisi mchana ambako kitakuwa kinasafiri kwa kilomita 170 kwa saa na kitakuwa kilomita 150 kutoka pwani ya Mtwara,”  alisema.

Aprili 23 Msemaji wa Taasisi ya Kupambana na Majanga wa Msumbiji, Paulo Tomás, alitangaza tahadhari ya uwezekano wa kutokea kimbunga hicho, akisisitiza kuwa wataendelea kufuatilia namna   mfumo wa hali hiyo ya hewa unavyoendelea kuibuka na kujipanga kadri inavyotakiwa.

Machi 14, baadhi ya maeneo ya Msumbiji, Malawi na Zimbabwe yalikumbwa na kimbunga Idai.

Kwa mujibu wa Kamati ya Dharura ya Majanga ya Uingereza, watu 960 walifariki dunia  kutokana na athari za kimbunga hicho. 

Mtandao uliobobea kwenye masuala ya hali ya hewa wa AccuWeather wa  Marekani pia uliripoti jana kuwa mwenendo wa mifumo ya hali ya hewa katika bahari ya Hindi  HYPERLINK “https://www.accuweather.com/en/weather-news/brewing-tropical-cyclone-to-threaten-mozambique-tanzania-later-this-week/70008064” huenda ukasababisha  kutokea kimbunga hicho kutokana na kuimarika  hali ya mgandamizo mdogo wa hewa.

Taarifa hiyo ilieleza kuwa iwapo kimbunga hicho kitatokea kama ilivyotarajiwa kuanzia leo, kinatarajiwa kuathiri Lindi mpaka Pemba I  Kaskazini mwa Msumbiji.

“Mvua kali  inayoweza kusababisha mafuriko na mmomonyoko wa udongo katika maeneo kama Masasi na Tunduru nchini Tanzania, pia Marrupu na Montepuez  kwa upande wa Msumbiji,” ilieleza taarifa ta AccuWeather.

Mtwara hali si shwari

Akizungumzia kimbunga hicho, Meneja wa Mamlaka ya Hali ya Hewa Kanda ya Kusini, Daudi Amasi, alisema kimbunga hicho kitasababisha  upepo mkali, radi, mvua kubwa, kuchafuka kwa mawimbi ya bahari na bahari kujaa hali ambayo inaweza kuathiri wanaoishi kando ya bahari.

Alisema tahadhari kubwa inapaswa ichukuliwe kwa wakazi wa mabondeni kuhama huku meneo yenye mifereji yakisafishwa na kuondolewa taka kuruhusu maji kupita kwa urahisi.

“Hali hii inaweza kuanza kesho asubuhi ambako mvua itanyesha mpaka   saa tatu na kufikia saa tano hadi saa sita mvua itazidi na  itanyesha mpaka saa tisa usiku.

“Majira hayo mvua itaanza kupungua na kitakuwa kikiondoka kuelekea  Msumbiji, kwa siku ya kesho usafiri wa majini na anga hautarajiii kuwapo hadi kimbunga hicho kipite.

 “Hiki kimbunga kinakuja kwa kasi ya kilomita 76 hadi sasa bado tunaendelea kuangalia kuona kama kinaweza kuongezeka nguvu na kikiongeza nguvu kinaweza kuleta madhara makubwa zaidi,” alisema. 

Akizungumzia taarifa za kimbunga hicho, Mkuu wa Mkoa wa Mtwara, Gelasius Byakanwa, alisema wataalamu wameona kuja kwake kikiwa na uelekeo wa mkoa wa Mtwara na kinaweza kuleta madhara makubwa.

Kwa upande wa wananchi, Sophia Likwanda mkazi wa Nandope Manispaa ya Mtwara Mikindani alisema   kitendo cha kusikia  a kimbunga hicho amejikuta katika wakati mgumu kutokana na eneo ambalo nyumba yake ilipo.

Mkazi wa Nandope, Iddi Mapira alisema ni vema Serikali ichukue tahadhari mapema   kuwanusuru wananchi na majanga yatakayoweza kujitokeza endapo kimbunga hicho kitatokea.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles