26.9 C
Dar es Salaam
Saturday, November 30, 2024

Contact us: [email protected]

Kimbunga cha ubunge chawakumba vigogo CUF

Adam Mkwepu na Michael Sarungi Dar es Salaam
WAJUMBE wa Mkutano Mkuu wa Chama cha Wananchi (CUF) wa wilaya za Kinondoni, Temeke na Ilala wamefanya uchaguzi wa kura za maoni na kuwapata wawakilishi wao katika uchaguzi ujao katika nafasi za ubunge wa majimbo na viti maalumu Mkoa wa Dar es Salaam.
Mmikutano hiyo ya kura za maoni imeacha vilio kwa vigogo wa chama hicho, akiwamo Naibu Mkurugenzi wa Habari na Uenezi, Abdul Kambaya aliyejikuta akibwagwa na Naibu Katibu Mkuu wa Jumuiya ya Vijana wa chama hicho, Maulid Saidi.
Akitangaza matokeo hayo, Msimamizi wa kura hiyo ya maoni, Masoud Mhina, alimtangaza Maulidi kuwa mshindi kwa kupata kura (88), Kambaya (61), Karama Masoud ‘Kalapina’ (8) na Faraji Rangi akiambulia kura moja.
Alisema kwa mujibu wa katiba ya chama hicho majimbo mengine ya Ubungo na Kawe hayakufanya uchaguzi kwa sababu wagombea waliojitokeza kuwania nafasi hizo ni mmoja kwa kila jimbo kwa hiyo wamepita na majina yao yatasonga mbele kwenye vikao vya juu.
Kwa ubunge wa viti maalumu, aliyechaguliwa ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji wa Wilaya ya Kinodnoni, Blandina Mwasabwite (90) mpinzani wake Hawa Masoud (60).
Kwa Wilaya ya Temeke hasa katika jimbo la Temeke, ambalo lilikuwa na wagombea tisa, Mkurugenzi wa Mambo ya Nje wa CUF, Abdallah Mtolea (120), akiwashinda Hafidhi Faki na Shabani Kaswaka.
Jimbo la Kigamboni lilikuwa na wagombea wawili ambako Mwenyekiti wa CUF Wilaya ya Kinondoni, Juma Nkumbi, alishinda kura za maoni kwa kupata kura (131) akimshinda mpinzani wake Kondo Bungo (72).
Pamoja na kuibuka kwa upinzani, hali ilikuwa tofauti kwa aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CUF Bara, Julius Mtatiro ambaye alishinda kwa kura (38) dhidi ya Mjumbe wa Baraza Kuu la Uongozi la Taifa la chama hicho, Ashura Mustapha.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles