23.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 28, 2023

Contact us: [email protected]

KIMBUNGA CHA AJABU CHASOMBA MWANAFUNZI MBEYA

Na Ibrahim Yassin, Mbeya

KATIKA hali isiyo ya kawaida kimbunga cha ajabu kimembeba mwanafunzi wa kidato cha nne Happy Michael Mwakabenga akiwa ameshika jagi akipiga mswaki mtaa wa Maendeleo Kata ya Iyunga Jijini Mbeya na kuzua taharuki kubwa mtaani hapo.

Akizungumza kwa masikitiko jana na gazeti hili,Happy alisema tukio hilo lilitokea alasiri akiwa nyumbani kwao akipiga mswaki wakati mama yake akiwa ndani alijikuta ghafla amesombwa na kimbuka hicho.

Alisema wakati anasombwa hakujielewa kwani alikuja kujielewa akiwa mbali na eneo la nyumbani kwao huku jagi na mswaki vikiwa vimeangukia sehemu nyingine.

Kutokana na tukio hilo Happy amevunjika mguu wa kulia na tayari amepatiwa matibabu hali yake inaendelea vizuri.

Mama mzazi wa Happy, aliyetambulika kwa majina ya

Scolla Alex alisema akiwa ndani ghafla alisikia kishindo na kelele za mwanae alipotoka hakumuona ndipo hofu ilipozuka.

Alisema baada ya tukio hilo alipiga mayowe yaliyokusanya watu wakiwemo ndugu na kuanza kumtafuta hadi walipo mpata akiwa hajitambui kilometa 2 kutoka katika nyumba yao.

Shangazi wa mwanafunzi huyo, Sophia Mwakabenga akiwa na na jirani yake Bombaga Kitwika baada ya kufika eneo hilo,kwa nyakati tofauti walilihusisha tukio hilo na iamani za kishirikina.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Mtaa wa Maendeleo Kata ya Iyunga, Elias Mwakyusa pamoja na kusikitishwa na tukio hilo pia aliwatoa hofu wananchi wake akisema kuwa ni hali ya hewa tu imesababisha  kutokea tukio hilo na kusema kuwa ni jambo la kawaida.

Mtaa wa Maendeleo umekuwa na matukio mengi yanayotaatanisha yakiwemo ya watoto kutoweka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,745FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles