22.6 C
Dar es Salaam
Tuesday, September 17, 2024

Contact us: [email protected]

Kim: Napenda mwanangu aitwe Easton

kim-kardashian_glamour_2apr15_getty_b_720x1080NEW YORK, MAREKANI

MKE wa msanii wa hip hop nchini Marekani, Kanye West, Kim Kardashian, amesema anapenda mtoto wake aje aitwe Easton tofauti na jina lingine.

Mtoto wake wa kwanza amepewa jina la North huku baba yake akiitwa West, hivyo watu wengi wakijiuliza jina la mtoto ajaye ataitwa nani kati ya East au South, lakini mama huyo amesema angependa mtoto huyo aitwe Easton.

“Ningependa mtoto huyo aje aitwe Easton, lakini sina uhakika kama mume wangu atakubaliana na mimi.

“Sina uhakika kama atakuwa na lengo la kutoa jina la mwelekeo kama ilivyo kwake West na mtoto akiitwa North, watu wengi wanadhani kuwa ataiwa South.

Hata hivyo, mama huyo amesema mpaka sasa bado yeye na mume wake hawajapanga jina la mtoto huyo ambaye wanamtarajia hivi karibuni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles