25.3 C
Dar es Salaam
Monday, January 17, 2022

KIM KARDASHIAN KULIPA CHOCHOTE ILI APATE MTOTO WA TATU

NEW YORK, MAREKANI


MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, ameweka wazi kuwa yupo tayari kutumia kiasi chochote cha fedha ili mfuko wake wa uzazi usafishwe, apate ujauzito wa mtoto wa tatu.

Kwa sasa mrembo huyo ambaye ni mke wa rapa Kanye West, aligundulika kuwa na matatizo ya kizazi baada ya kumpata mtoto wa pili mwaka jana.

Lakini Kim alidai yupo tayari kutumia kiasi chochote cha fedha kwa madaktari watakaoweza kusafisha mfuko wake wa uzazi na akapata mimba kwa kuwa lengo lake ni kuwa na familia kubwa.

“Napenda sana watoto, nataka kuwa na familia kubwa, hivyo natafuta wataalamu watakaoweza kusafisha mfuko wangu wa uzazi ili nipate ujauzito wa mtoto mwingine, imani yangu ni kwamba jambo hilo litawezekana,” alisema Kim.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
174,717FollowersFollow
531,000SubscribersSubscribe

Latest Articles