22.8 C
Dar es Salaam
Thursday, October 6, 2022

KIM KARDASHIAN ATINGA IKULU KUTETEA WANAWAKE

NEW YORK, MAREKANI

MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani, Kim Kardashian, ameweka wazi sababu za kwenda Ikulu kukutana na rais Donald Trump kwa mara ya kwanza.

Katikati ya wiki hii mrembo huyo alikutana na Trump na kumweleza kuwa wanawake wengi nchini humo wamekuwa wakikosa uhuru wa kufanya mambo yao, hivyo wanaomba wapewe uhuru.

Hata hivyo Kim alitumia muda wake kumwomba rais atumie busara zake na kumpunguzia kifungo kama siyo kumwachia huru mwanamama Alice Marie Johnson, ambaye anatumikia kifungo cha maisha kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya.

“Napenda kutumia nafasi hii kumshukuru Rais kwa kukubali ombi langu la kwenda kuonana Ikulu, ninaamini anaweza kuyafanyia kazi yale yote ambayo nimemueleza,” alisema Kim Kardashian.

Mashabiki wengi wanaamini kwa ukaribu wa rais Trump na familia ya Kanye West, unaweza kumfanya rais huyo kuyakubali maombi ya Kim.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,814FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles