Kim: Kanye West sikumuiba kwa Amber Rose

0
732

LOS ANGELES, MAREKANI

MWANAMITINDO Kim Kardashian, amefunguka kwa mara ya kwanza akikanusha kumuiba mume wake Kanye West kwa mwanamitindo Amber Rose.

Rapa Kanye West kabla ya kufunga ndoa na Kim, alikuwa kwenye uhusiano na Amber Rose, lakini baada ya kuachana ndipo Kim akaingia kwenye uhusiano na kisha kufunga ndoa.

“Dunia yote inajua kama nilimuiba Kanye West kutoka kwa Amber Rose, hii sio kweli nina risiti kabisa, wao waliachana na baadae tukaja kuanzisha uhusiano wetu.

“Familia yetu imekuwa ikizungumziwa hivyo, hivi ni kweli Khloe alimuiba Tristan Thompson kutoka kwa Jordan Craig? Sio kweli, wakaja kusema tena kuwa, Khloe alimuiba French Montana kutoka kwa Trina, ukweli ni kwamba wanaume hao walimfuata na sio yeye kuwafuata,” alisema Kim

Kim baada ya kuingia kwenye uhusiano na Kanye West, walifanikiwa kufunga ndoa Mei 2014 na hadi sasa wana jumla ya watoto wanne.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here