20.5 C
Dar es Salaam
Saturday, August 20, 2022

KIM, KANYE WATARAJIA MAPACHA

CALIFORIA, MAREKANIMKALI wa muziki wa hip hop nchini Marekani, Kanye West na mke wake, mwanamitindo Kim Kardashian, wanatarajia kupata watoto wawili mapacha kwa njia ya upandikizaji.

Kim alishauriwa asishike tena mimba kutokana na kuwa na tatizo la kizazi, hivyo mrembo huyo na mume wake bado wanahitaji familia yao kuwa kubwa, ingawa hadi sasa wana watoto wawili.

Kutokana na hali hiyo, wameamua kutumia fedha zao ili kupandikiza mbegu zao kwa mwanamke mwingine na wamethibitisha kuwa wanatarajia watoto wawili mapacha mapema mwakani.

Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Kim amedai ana furaha kubwa, kwa kuwa familia yake itakuwa kubwa tofauti na vile watu wanavyodhani.

“Nani anajua nini kinakwenda kutokea? Furaha yetu ni kuona tunakuwa na familia kubwa kama inavyokwenda kutokea mapema mwakani, tunatarajia kuongeza watoto wawili,” alisema Kim.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
199,058FollowersFollow
551,000SubscribersSubscribe

Latest Articles