29.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 18, 2021

Kim, Kanye wanaswa tena

KIM Kardashian na Kanye West wamerudiana? Hilo ndilo swali linaloendelea kuumiza vichwa vya wapenzi wa habari za mastaa baada ya wawili hao kunaswa wakiwa pamoja.

Inaeleweka kuwa Kim na Kanye waliachana miezi michache iliyopita lakini hii ya kuonekana wakiwa wametoka kupata chakula cha usiku katika moja ya migahawa maarufu mjini Malibu, Marekani.

Hata baada ya kupata msosi, walipanda gari moja na kutokomea wakiwa na marafiki zao, jambo lililoacha minong’ono kuwa wamerudiana.

Kuachana kwao ilikuwa habari kubwa mwanzoni mwa mwaka huu, ikikumbukwa kuwa waliishi kwenye ndoa yao kwa miaka saba.

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

66,457FansLike
162,310FollowersFollow
522,000SubscribersSubscribe

Latest Articles