Kim aanika kinachomsumbua Kanye West

0
899

LOS ANGELES, MAREKANI 

MKE wa rapa Kanye West, Kim Kardashian, amefunguka kwa mara ya kwanza kinachomsumbua mumewe ni tatizo la afya ya akili maarufu kama Bipolar.

Hivi karibuni Kanye West akiwa kwenye uzinduzi wa kampeni ya kuwania urais wa nchi hiyo alizungumzia suala la utoaji mimba, ambapo aligusia kisa cha baba yake kutaka kumtoa aalipokuwa kwenye tumbo la mama yake na yeye pia alitaka kuchomoa ujautizo wa mtoto wao wa kwanza jambo lililomfanya alie kama mtoto mpaka watu wakaanza kushangaa.

Aidha Kanye West alihamia katika ukurasa wa Twitter ambapo kwa siku mbili mfululizo alikuwa anaandika mambo ambayo hayaeleweki akiwachana watu tofauti akiwamo mkwe wake, Kris Janner na rapa Meek Mill aliyehisi anatoka kimapenzi na mkewe.

 “Kama ambavyo wengi wenu mnafahamu, Kanye anasumbuliwa na bipolar. Mtu yeyote ambaye ana ugonjwa huu au mpendwa wake, anajua namna ambavyo inasumbua na maumivu yake yalivyo lakini tumekuwa kimya kwa kipindi kirefu kwa ajili ya familia yetu ila ukweli ndio huo, hivyo anaweza kufanya jambo likashangaza kidogo,” alisema Kim.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here