25.4 C
Dar es Salaam
Monday, January 30, 2023

Contact us: [email protected]

KILO 99 DAWA ZA KULEVYA ZAKAMATWA DODOMA

Na SARAH MOSES, DODOMA

KILO 99 za dawa za kulevya zimekamatwa mkoani hapa.

Taarifa hiyo ilitolewa juzi na Mkuu wa Wilaya ya Dodoma Mjini, Christina Mndeme, alipokuwa akizungumza na wenyeviti wa mitaa pamoja na watendaji mjini hapa.

Alisema kuwa, Wilaya ya Dodoma ndiyo inayotumiwa na wafanyabiashara hao, kupokea dawa hizo kutoka katika mikoa mbalimbali nchini.

“Kuna kesi 168 zinazowakabili watu 240 kwa utumiaji na uuzaji wa dawa za kulevya. Hivyo basi, nyie viongozi watajeni watu wote wanaojihusisha na biashara hiyo hata kama ni wanasiasa au watu wenye uwezo kifedha,” alisema Mndeme.

Aliyataja maeneo yanayoongoza kwa kuuza dawa hizo za kulevya kuwa ni Miyuji, Hazina, Airport, Mlezi na Chinangali West.

Kwa upande wake, Mkuu wa Polisi Wilaya ya Dodoma Mjini, Daniel Shillah, aliwataka wananchi kuwa makini na watu waliowapangisha kwenye nyumba zao kwani wengi wao wanajihusisha na uuzaji wa dawa za kulevya.

“Wenyeviti ninyi mnawajua vizuri wananchi wenu, hivyo basi kuweni makini nao na kama kuna mtu unajua anatumia au anauza, njoo utoe taarifa na sisi Jeshi la Polisi tutamshughulikia.

“Adhabu ya mtu ambaye nyumba yake itakutwa na dawa za kulevya, atatozwa faini ya shilingi milioni moja kwa kuruhusu nyumba yake iwe na dawa hizo na mtumiaji atatozwa faini ya shilingi milioni tatu.

“Kwa kifupi ni kwamba, Wilaya yetu ya Dodoma Mjini inaongoza kwa kuwa na bangi pamoja na mirungi na maeneo yaliyoathiriwa na dawa hizo ni pamoja na Makutupora, Msalato, Veyula, Kizota, Majengo, Mailimbili, Chadulu, Zuzu, Bahiroad na Mbabala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles