29.8 C
Dar es Salaam
Sunday, September 15, 2024

Contact us: [email protected]

Kill MediaAir wampa tano Rais Samia kwa kutoa fursa za utalii kwa Vijana

Na Esther Mnyika, Mtanzania Digital

Wadau wa Sekta ya Utalii nchini wameipongeza Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na Rais Dk. Samia Suluhu Hassan kwa namna ambavyo imeendelea kutoa fursa kwa vijana hasa katika nyanja ya utalii.

Pongeze hizo zimetolewa Oktobab 6, 2023 na Mkurugenzi Mtendaji wa Kampuni inayojihusisha na kuangalia usalama wa watalii waotembelea nchini ya Kili MediAir, Dk. Hussein Abradha kwenye maonyesho ya Saba ya S!TE yanayoendelea katika Ukumbi wa Mlimani City jijini Dar es Salaam.

Amesema wanaipongeza Serikali ya Dk. Samia kwa namna ambavyo imeendelea kutoa fursa kwa vijana na kuitangaza nchi.

“Kili MediAir unaishukuru Serikali ya Awamu ya Sita inayoongozwa na mama yetu Rais Dk. Samia Suluhu Hassan katika kuhakikisha kwamba tunashiriki kwenye fursa za utalii moja kwa moja.

“Kili MediaAir tumejipanga kuhakikisha utalii wetu unazidi kupamba moto nchini kwa kuangalia eneo hili la usalama, hivyo tumejipa jukumu la kuhakikisha kwamba watalii wnaoingia nchini wanakuwa salama mpaka wanaondoka hii inahusisha afya ya mtalii na majanga yoyote ambayo anaweza kuyapata pindi anapokuwa kwenye vivutio vyetu,” amesema Dk. Abradha.

Aidha, ametoa rai kwa watalii kujitokeza kwa wingi nchini kuja kuangalia vivutio vilivyopo kwani nchi ipo salama na usalama wa mtalii umezingatiwa.

Taasisi ya kilimediAir inajishughulisha na usalama wa watalii katika vivutio na kwa sasa imejikita zaidi Kaskazini huku wakiwa na malengo ya kufikia vivutio vyote nchini.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles