25.4 C
Dar es Salaam
Saturday, November 16, 2024

Contact us: [email protected]

Kilimanjaro Stars kumekucha

Na THERESIA GASPER-DAR ES SALAAM

KOCHA Mkuu wa timu ya Taifa ya Tanzania Bara, Kilimanjaro Stars, Etienne Ndayiragije, amesema wachezaji wote waliopo kambini wapo fiti na wameanza mahesabu kuhakikisha wanafanya vizuri kwenye michuano ya Chalenji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati (Cecafa).

Michuano hiyo inatarajia kuanza kufanyika Desemba 9 hadi 19, mwaka huu nchini humo, ambako zitashirikisha timu 10.

Timu hizo zipo kwenye makundi matatu ambako Kundi A ni Uganda, Burundi, Ethiopia, na Eritrea, huku Kundi B zikiwa DRC Congo, Sudan, South Sudan na Somalia na Kundi C ni Kenya, Tanzania, Djibout na Zanzibar.

Akizungumza na MTANZANIA jana, Ndayiragije alisema, wachezaji aliowaita wameingia kambini na jana walianza mahesabu kuhakikisha wanaenda kwa kishindo katika michuano hiyo.

“Tumeanza kambi tangu Jumapili jioni na leo (jana) tutaanza mazoezi, hadi sasa sijapata taarifa yoyote kama kuna mchezaji ambaye ni majeruhi,” alisema.

Alisema wachezaji wote wamefika hadi wale wa nje isipokuwa Eliud Ambokile ambaye hadi jana alikuwa hajaungana na wenzake.

Timu hiyo inaendelea na mazoezi katika dimba la Taifa ikiwa ni maandalizi kabla ya kuanza safari ya kwenda Uganda.

Wachezaji walioitwa katika kikosi hicho ni Makipa Juma Kaseja (KMC), Metacha Mnata (Yanga), Aishi Manula (Simba) na David Kisu (Gor Mahia, Kenya).

Mabeki ni Juma Abdul, Kelvin Yondan (Yanga), Nickson Kibabage (Difaa El Jadida, Morocco), Gadiel Michael, Mohammed Hussein ‘Tshabalala’, (Simba), Mwaita Gereza (Kagera Sugar) na Bakari Mwamnyeto (Coastal Union).

Viungo ni Abdulmajid Mangalo (Biashara United), Jonas Mkude, Mzamiru Yassin, Hassan Dilunga (Simba), Fred Tengelu, Paul Nonga (Lipuli FC), Zawadi Mauya (Kagera Sugar), Idd Seleman, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ (Azam FC), Kelvin John (Football House), Ditram Nchimbi (Polisi Tanzania), Mkandala Cleofance (Tanzania Prisons) na Jafar Kibaya (Mtibwa Sugar).

Washambuliaji ni Eliud Ambokile (TP Mazembe, DR Congo), Miraji Athuman (Simba), Yusuph Mhilu (Kagera Sugar), Eliuter Mpepo (Buildcon, Zambia), Shaban Chilunda (Azam FC) na Kikoti Lucas (Namungo FC).

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
591,000SubscribersSubscribe

Latest Articles