30.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kilimanjaro QueensVs Kenya tena fainali Cecafa

NA SOSTHENES NYONI-DAR ES SALAAM

TIMU ya Taifa ya Wanawake ya Tanzania ‘Kilimanjaro Queens’ imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Uganda, katika mchezo wa nusu fainali ya michuano ya Chalenji ya nchi za Afrika Mashariki na Kati, uliochezwa jana jioni Uwanja wa Azam Complex, Dar es Salaam.

Michuano hiyo imeandaliwa na Baraza la Vyama Vya Soka kwa nchi za Afrika Mashariki na Kati(Cecafa).
Katika mchezo huo, Kilimanjaro Queens ililazimika kusubiri hadi dakika ya 90 kupata bao lililoipa ushindi lililofungwa na nahodha wake Asha Mwalala.

Asha alifunga bao hilo  lililomaliza ndoto za Uganda kutinga fainali, baada ya kupokea pande safi la winga Mwanahamisi Omari .

Fainali ya michuano hiyo itapigwa Jumatatu katika dimba hilo la Azam Complex.

Katika mchezo mwingine wa nusu fainali uliochezwa kuanzia saa nane mchana, Kenya ilitakata kwa ushindi wa mabao 5-0 dhidi ya Burundi.

Hiyo itakuwa mara ya tatu kwa Kilimanjaro Queens na Kenya kukutana fainali ya michuano hiyo, huku mara mbili zote Tanzania ikifanikiwa kuibuka kidedea.

Mara ya mwisho michuano hiyo ilifanyika nchini Uganda, ambapo Kilimanjaro Queens iliibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Kenya na kutwaa ubingwa.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles