26.2 C
Dar es Salaam
Thursday, June 1, 2023

Contact us: [email protected]

Kikwete awataka watanzania kusherekea sikukuu bila kuharibu funga zao

Na Brighiter Masaki
-Dae at es Salaam.

Rais Mstaafu wa awamu ya nne Dkt Jakaya Mrisho Kikwete, awataka wananchi wa Tanzania, kusherekea Sikukuu ya Iddi kwa amani bila kuharibu fungal zao.

Akizungumza wakati wa Iftari iliyoandaliwa na Banki ya Taifa ya Biashara, NBC usiku wa kuamkia Leo, jijini Dar es Salaam, Raid Msataafu Kikwete amesema waislamu na watanzania wajiandae kusherekea sikukuu wa amani.

Amesema kuwa ingekuwa kipindi cha aliyekuwa Mtabiri maarufu nchini wa Afrika na Dunia Marehemu Shekh Yahya angetuambia idadi ya waliofunga ni wangapi? Kwa kuwa Alishawai kutuambia kuwa katika funga yote walifungu watu wawili.

Aidha amewapongeza Bank ya Taifa ya Biashara, NBC kwa kuweza kufuturisha waliofunga na kwakuwa wanapata sawabu sawasawa na waliofunga.

“Niwapongeze kwa kuweza kufuturisha na Mwenyezi Mungu awabariki kwa mlichokifanya ni kitu kikubwa sana, kuna wengi hawajafikiria kuweza kuwafuturi lakini ninyi mmeweza bila kuangalia” amesema Kikwete

“Nipende kuwatakia sikuu njema watanzania, msherekee kwa amani bila kusahau kuharibu funga zengu mlizofunga kwa kipindi chote” amesema

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Taifa ya Biashara, NBC Theobald Sabi, amewashukuru wateja na wageni waliofika kwenye Iftari hiyo na kuwaomba waendelee kutumia Bank ya NBC.

” Bank yetu inatoa huduma nzuri na tunajali wateja wetu, tunakushukuru Rais Mstaafu wa Jamuhuri ya Muunganobwa Tanzania awamu ya nne kwa kukubali kushiriki pamoja nasi katika Iftari tulioiandaa”amesema Sabi

Kwa upande wake Mkurugenzi Mtendaji wa Banki ya Taifa ya Biashara NBC. Nd Theobald Sabi, aliwashukuru wateja na wageni waliofika kwenye Iftari hiyo na kusema kwamba ni mmoja ya matukio muhimu katika kalenda ya benki hiyo na ni sehemu ya kuongeza uhusiano na ushirikiano na wateja wao.

“Kwa muda mrefu benki yetu ya NBC imekuwa na utaratibu wa kuandaa futari kwa wateja wake Tanzania bara na visiwani Zanzibar wakati wa mwezi mtukufu wa Ramadhani.” alisema Sabi

Aidha Mkurugenzi Mtendaji wa NBC, Theobald Sabi aliongeza kuwa benki hiyo ina huduma za kibenki zinazofuata taratibu za Sharia. “ Huduma zetu za Islamic Banking zilianziswha. tangu mwaka 2010 na ni huduma za mbadala kwa wateja wetu wanaopenda kufanya miamala kwa kuzingatia sheria za Kiislamu. Huduma hizi zinawalenga wateja wakubwa, wadogo na wateja binafsi na zinapoatikaa katika matawi yote ya benki hiyo nchini.”

Baadhi ya huduma alizogusia ni mikopo isiokuwa na riba na inayofuata sheria kwa wafanyabiashara na waajiriwa, huduma za amana za muda maalum zenye gawio la faida halali na Akaunti ya Akiba ya La Riba iliyounganishwa na mfuko wa bima wa Takahul inayochangia hadi 1m ya rambi rambi kwa wanafamilia inpotokea mteja amefariki.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,225FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles