KIKOSI CHA STARS KITAKACHOONDOKA KUELEKEA UGANDA KESHO      

0
1196Na Lulu Ringo,Dar es Salaam

Timu ya Taifa (Taifa Stars) inatarajia kuondoka kesho saa saba mchana kuelekea Uganda ikiwa na jumla ya wachezaji 23.

Wachezaji hao ni, Golikipa Aishi Manula (Simba, Salum Kimenya(Tz Prisons),Frank Domayo(Azam FC), Salum Kihimbwa(Mtibwa),Kelvin Sabato(Mtibwa), David Mwantika(Azam FC) ,Ally Abdulkarim(Lipuli),Mohamed Abdulrahiman (JKT Tanzania ),Beno Kakolanya (Young Africans ),Hassan Kessy (Nkana,Zambia), Gadiel Michael (Young Africans), Abdi Banda (Baroka,Afrika Kusini), Aggrey Morris (Azam FC), Andrew Vicent (Young Africans ), Himid Mao (Petrojet,Misri),Mudathir Yahya (Azam FC),Simon Msuva (Al Jadida,Morocco), Rashid Mandawa (BDF,Botswana), Farid Mussa (Tenerife,Hispania), Mbwana Samatta (KRC Genk,Belgium), Thomas Ulimwengu (Al Hilal,Sudan), Shabani Chilunda (Tenerife,Hispania) naYahya zaydi(Azam FC).

Aidha kikosi hicho kitaambatana na viongozi, kocha Mkuu Emmanuel Amunike na wasaidizi wake Hemed Morocco na Emeka Amadi,Mtunza Vifaa Ally Ruvu na madaktari wawili Richard Yomba na Gilbert Kigadya.

Stars wanatarajia kushuka dimbani septemba 8 kuchuana na timu ya taifa ya Uganda (The Cranes),  katika michuano ya kuwania tiketi ya kushiriki (Afcon) mwakani.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here