26.2 C
Dar es Salaam
Monday, October 3, 2022

KIKONGWE ATARAJIA MTOTO

NEW YORK, MAREKANI


MKE wa zamani wa staa wa filamu nchini Marekani, Sylvester Stallone ‘Rambo’, Brigitte Nielsen, anatarajia mtoto wa tano huku akiwa na umri wa miaka 54.

Mwanamama huyo ambaye pia ni nyota wa filamu, ametumia ukurasa wake wa Instagram kuweka wazi kuwa anatarajia kuongeza mtoto wa tano bila ya kujali umri wake kuwa mkubwa.

“Familia inatarajia kuwa kubwa, nina furaha kuona inakuwa hivyo,” aliandika mama huyo mara baada ya kuposti picha yake akionesha jinsi tumbo lake lilivyo.

Kwa sasa Brigitte anaishi na mtayarishaji wa vipindi vya runinga nchini Italia, Mattia Dessi, mwenye umri wa miaka 39, baada ya kufunga ndoa mwaka 2006.

Hata hivyo, wataalamu wa afya wameweka wazi kuwa ni hatari kiafya kwa mwanamke kupata ujauzito kuanzia umri wa miaka 50.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
202,573FollowersFollow
554,000SubscribersSubscribe

Latest Articles