Na Mwandishi Wetu, Mtanzania Digital
Chuo cha Utumishi wa Umma Tanzania (TPSC) ni taasisi ya elimu ya juu nchini Tanzania chini ya Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, kilianzishwa mwaka 2000, kwa lengo la kutoa mafunzo kwa watumishi wa umma, kufanya tafiti mbalimbali, kutoa huduma za shauri elekezi na mafunzo bunifu kupitia teknolojia.
Adelaida Muganyizi ni Afisa Masoko Mkuu Mawasiliano na Masoko wa TPSC ambaye anasema kuwa chuo pamoja na kozi nyingine pia kimekuwa kikitoa mafunzo ya kuboresha utendaji wa watumishi wa umma.
“Taasisi yetu pia hutoa kozi mbalimbali kwa watumishi wa umma kulingana na uhitaji wa Taasisi husika, ili kuboresha na kuongeza ujuzi na maarifa kazini jambo ambalo limeongeza ufanisi wa watumishi wa umma,” anasema Adelaida.
Anasema kwasasa chuo hicho kina matawi sita pamoja na Kituo cha kuendesha mafunzo kwa njia ya mtandao kilichopo Dar es Salaam.
“Chuo hiki kina matawi sita katika maeneo yafuatayo: Tabora, Dar es Salaam,
Mtwara, Singida, Tanga na Mbeya, “Makao Makuu yapo Dar es Salaam Mtaa wa Bibi Titi Mohammed, mkabara na Chuo cha Biashara.
“Kwa mujibu wa muongozo wa chuo hicho maombi ngazi ya Cheti na Diploma dirisha la kwanza linafunguliwa Mei hadi Septemba na la pili linafunguliwa Januari hadi Machi huku maombi ya shahada ya kwanza yakiwa na dirisha moja la maombi.
Kwa mawasiliano zaidi tembelea tovuti yao ya www.tpsc.go.tz