30 C
Dar es Salaam
Friday, January 27, 2023

Contact us: [email protected]

KIJANA WA MIAKA 22 APAMBANA NA FISI

Na SEIF TAKAZA, SINGIDA


 

KIJANA mwenye umri wa miaka 22, Yusuf Ali, mkazi wa Kijiji cha Mgongo, Wilaya ya Iramba, Mkoa wa Singida, amepambana na fisi na kufanikiwa kumuua (22).

Tukio hilo lilitokea juzi kijijini hapo, baada ya fisi huyo kumvamia akiwa na wenzake wawili.

“Siku hiyo nilikuwa na wenzangu wawili tukitembea na ghafla tukamuona fisi akituangalia.

“Baada ya dakika chache, alituvamia na kuanza kuwashambulia wenzangu na kuwasababishia majeraha katika miili yao.

“Baada ya kuwajeruhi wenzagu, alinikimbiza na alipoanza kunishambulia, nilipata nguvu za ghafla na kuanza kupambana naye.

“Nilimkaba kabari ya shingo, kisha nikamshika mdomo kwa nguvu ili asiachame na wakati huo nilikuwa nikipiga kelele za kuomba msaada.

“Kutokana na kelele hizo, watu walikuja na kuanza kumkata na mashoka, mapanga na wengine kumpiga na marungu hadi akafa na hapo ndipo nikapumua na kumshukuru Mungu  kwa jinsi alivyoniokoa,” alisema kijana huyo.

Wakati huo huo, fisi wilayani humo, wanatishia maisha ya wakazi wa wilaya hiyo baada ya kujeruhi watu saba kwa nyakati tofauti.

MTANZANIA imeshuhudia majeruhi watano walioshambuliwa na mnyama huyo na kulazwa katika Hospitali ya Kiomboi na wengine wawili kuhamishiwa katika Hospitali ya Hydom, iliyoko Wilaya ya Mbulu, Mkoa wa Manyara.

Tukio la kwanza la mnyama huyo, lilitokea Februari 14, mwaka huu katika Kijiji cha Mgongo ambapo alijeruhi watu wanne.

Akizungumzia matukio hayo, Diwani wa Kata ya   Mukulu, Advesty Christopher, aliiambia MTANZANIA jana, kwamba Februari 16 mwaka huu, saa 11 jioni, fisi mmoja alijeruhi watu watatu na kuwasababishia maumivu makali.

“Nilipopata taarifa hiyo, nilikwenda moja kwa moja kwenye tukio katika Kitongoji cha Kagera (Mukulu D). Nilipofika mahali hapo, niliambiwa majeruhi walikuwa wamepelekwa Hospitali ya Wilaya ya Kiomboi.

“Lakini, kijijini hapo nilikutana na kijana mmoja anaitwa Ramadhani Kibuda ambaye alinisimulia jinsi tukio hilo lilivyokuwa.

“Alisema wakati wa tukio, yeye na wenzake walikuwa njiani wakitembea na walipomuona fsi huyo, aliwafuata na kuanza kuwashambulia mmoja baada ya mwingine, lakini yeye alinusurika baada ya kupanda kwenye mti,” alisema Diwani Christopher.

Naye Mganga Mfawidhi wa Hospitali ya Wilaya hiyo, Dk. Adam Mashenene, alithibitisha kupokea majeruhi waliofikishwa hospotalini hapo baada ya kujeruhiwa na fisi.

Alitaja majina ya majeruhi hao kuwa ni Yusuf Ali (22), Ramadhani Juma(65) na Charles Juma (42), alijeruhiwa usoni.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,063FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles