31.2 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kigwangala: Tumesambaratisha mitandao ya majangili

ELIYA MBONEA-ARUSHA

Waziri wa Maliasili na Utalii, Dk. Hamisi Kigwangala amesema mitandao ya ujangili imesambaratishwa na hivyo kufanya ujangili wa kibiashara kwa meno ya tembo na faru kupungua kwa asilimia 80.

Ameitoa Kauli hiyo hivi karibuni akiwa katika Kituo cha Mafunzo ya Awali ya Jeshi Usu Mbulumbulu kinachomilikiwa na Mamlaka ya Hifadhi ya Ngorongoro (NCAA) kilichopo wilayani Karatu mkoani Arusha.

Akifunga mafunzo ya awali ya Jeshi la Usu kwa askari 112 wa NCAA Kigwangala amesema ujangili umekwishakoma nchini kwani kesi wanazopata ni za meno ya tembo waliouawa miaka nane hadi 10 nyuma na kwa upande wa faru hawapati kabisa.

“Hakuna tembo wapya wanaouawa, mitandao yao tumeisambaratisha. nina uhakika tukichukua takwimu uwezekano mkubwa ujangili utakuwa umepungua kwa zaidi ya asilimia 80,” amesema Dk. Kigwangala.

Ameongeza kuwa asilimia 20 inayobakia kati ya 80 huenda ikawa kwa wanyamapori wanaovamiwa kwa bahati mbaya, uwindaji haramu wa nyama ya kitoweo na kuwekewa sumu wanapovamia mashamba ya watu.

“Tumekusudia ifikapo mwaka 2022 tusiwe tunazunguzia ujangili nchini, kwa niaba ya serikali niwapongeze wahifadhi wote na askari kwa kazi nzuri mnayoifanya chini ya ungozi wa Rais Dk. John Magufuli,” alisema Dk. Kigwangala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles