33.2 C
Dar es Salaam
Friday, March 29, 2024

Contact us: [email protected]

Kifusi chafukia watu 10 mgodini, mmoja afariki

YOHANA PAUL Na FATUMA SAID -MWANZA

MTU mmoja amefariki dunia na wengine nane kujeruhiwa, huku mmoja akiwa hajulikani alipo baada ya kufukiwa na kifusi katika mgodi wa dhahabu wa Shilalo uliopo Inonelwa, Wilaya ya Misungwi mkoani Mwanza.

Tukio hilo lilitokea juzi usiku wakati wakiendelea na shughuli za uchimbaji madini.

Imeelezwa kuwa baada ya wachimbaji kuingia ndani ya mashimo (mduara), ghafla kifusi kiliporomoka na kuwafukia watu 10 waliokuwamo ndani ya mgodi huo.

Aliyefariki dunia ni Ndaki Juma (45), mkazi wa Nyamikoma, Wilaya ya Busega mkoani Simiyu na majeruhi wametajwa kuwa ni Keo Werema, John Katwale, Mwita George, Masanja Charles, Abdallah Abdu, Bengwe Clement, Songa Charles, Emmanuel Mathias na Mangera Meki.

Akithibitisha kutokea tukio hilo, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Mwanza, Jumanne Muliro, alisema tayari majeruhi nane wameokolewa na kukimbizwa Hospitali ya Wilaya ya Misungwi kwa matibabu zaidi, huku mtu mmoja aliyefukiwa hajapatikana hadi sasa.

Kamanda Muliro alisema jeshi lake lilipokea taarifa za kutokea tukio hilo saa 7 usiku, ndipo askari kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama ya Wilaya ya Misungwi walifika haraka eneo la tukio.

“Jeshi la Polisi lilipokea taarifa za tukio la kuporomoka mgodi wa Shilalo, askari wetu kwa kushirikiana na Kamati ya Ulinzi na Usalama tulifika mapema eneo la tukio na kufanikiwa kuwaokoa watu wanane, mmoja akiwa amefariki dunia na mwingine hajapatikana.

“Majeruhi wote wamepelekwa Hospitali ya Wilaya Misungwi na juhudi za kumtafuta mwenzao  zinaendelea kufanyika,” alisema Kamanda Muliro.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
585,000SubscribersSubscribe

Latest Articles