UN, NEW YORK
AZIMIO limewasilishwa Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa likitaka uchunguzi kuhusu ajali ya ndege iliyotokea mwaka 1961 na kusababisha kifo cha aliyekuwa Katibu Mkuu wa Umoja wa Mataifa (UN) wakati huo, Dag Hammarskjold.
Ndege hiyo ilianguka eneo ambalo kwa sasa ni nchi ya Zambia, wakati wa ziara ya kidiplomasia kujaribu kuleta usitishwaji wa vita ya wenyewe kwa wenyewe nchini Congo.
Wakati huo, makosa ya rubani yalitajwa kuwa sababu ya kuanguka kwa ndege hiyo, lakini pia kukiibuka ushahidi mpya ambao huenda ukaongeza shaka kuwa ajali hiyo ilipangwa.