26.9 C
Dar es Salaam
Friday, December 9, 2022

Contact us: [email protected]

Kiduku: Mwakinyo hauwezi muziki wangu

Na GLORY MLAY-DAR ES SALAAM

BONDIA wa ngumi za kulipwa hapa nchini, Twaha Kiduku, amesema yupo tayari kupanda ulingoni na Hassan Mwakinyo, ili kuwathibitishia Watanzania kuwa yeye ndiyo mbabe kati yao.

Akizungumza na MTANZANIA jana jijini hapa, Kiduku, alisema kuwa  pambano hilo litakuwa kivutio kwa watu wengi hasa mashabiki wa ngumi, lakini pia litamuongezea heshima Mwakinyo kama akifanikiwa kumpiga .

Alisema kuwa anajiamini na hakuna bondia anayeweza kumpiga kwani wengi wao wamekuwa wakimkimbia.

“Hata kesho nipo tayari kuzichapa na Mwakinyo, kwanza atajipatia umaarufu akipiga mimi, siogopi bondia yoyote najiamini kwa sababu hii ni kazi ambayo inaniweka hapa mjini na kuisaidia familia yangu.

“Mazoezi ninayofanya hakuna bondia mbaye anayafanya si ya kitoto, kocha wangu ananipa mbinu ambazo sodhani kama nikipanda ulingoni Mwakinyo atachomoka,” alisema.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
205,735FollowersFollow
558,000SubscribersSubscribe

Latest Articles