KIDOA: ANAYENITAKA AJE NA MABUNDA TU

0
1631

kidoa

Na KYALAA SEHEYE,

STAA anayepamba video za wasanii mbalimbali wa Bongo Fleva a.k.a Video Queen, Asha Salum ‘Kidoa’ amefunguka kuwa malipo kidogo anayopata kutokana na kazi hiyo yamemfanya aamue kukaa pembeni na kugeukia uigizaji.

Akizungumza na Gumzo la Town la Mtanzania Jumamosi, Kidoa amesema kwa sasa yupo bize zaidi katika uigizaji wa tamthilia na filamu mbalimbali.

Anasema: “Hakuna kitu kwenye u-Video Vixen, tunalipwa kidogo sana. Kwa sasa sitaki tena. Naweza kusema hakuna cha maana zaidi ya kuonekana… lakini kama mtu akija na pesa ya maana, naweza kushiriki kwenye video yake.”

Alipoulizwa pesa ya maana ni kiwango gani, haraka alisema: “Pesa ya kueleweka. Nimechoka kufanya kazi isiyokuwa na malengo, mtu akija na milioni yake, naingia mzigoni. Chini ya milioni moja, sishiriki video ya msanii kabisa.”

TAMTHILIA DILI ZAIDI

“Niseme ukweli, kwa sasa najivunia nimekuwa hot cake kwenye tamthilia… natafutwa sana na ninafanya kazi hata  tano ilimradi tukubaliane.

“Ujue tamthilia na filamu wananilipa vizuri sana, pesa ambayo sijawahi kulipwa na ninahisi huko kwenye video za wasanii sikuwahi kufikiria kupata fedha kama hizi, ndiyo maana nimefumbuka macho na kuitambua thamani yangu,” anasema.

MWANZO WALIMKATAA

Anasema pamoja na kwamba kwa sasa amepata mapokezi mazuri na makubwa kwenye tamthilia na filamu, awali walimgomea wakidhani hana kipaji.

“Mimi kipaji changu hasa ni uigizaji, sikuwa na ndoto za kuwa Video Vixen kabisa. Niliwafuata baadhi ya wasanii na watayarishaji wakubwa lakini walinitosha wakiamini labda sina kipaji, lakini leo hii wameona uwezo wangu wamenikubali.

“Siwezi kukataa kuwa video za wasanii wa Bongo Fleva zimenisaidia, kwakweli zimenitoa lakini hazilipi. Maisha siyo kuonekana tu, lazima uwe na kitu unaingiza ndiyo utaona raha ya kazi,” anasema Kidoa ambaye video ya  Akadumba ya msanii Ney wa Mitego ndiyo iliyomtambulisha.

BIFU NA MASOGANGE

Iliwahi kuripotiwa kuwa, Kidoa alikuwa kwenye bifu zito na mrembo  mwenzake, Agnes Gerald maarufu Masogange, kisa kikielezwa ni kugombea penzi la staa wa filamu za Kibongo, Rammy Galis; Kidoa anasema juu ya hilo?

“Ni kweli tulikuwa na bifu tena kubwa sana lakini tulikuja kukaa tukaelewana. Unajua ilivyo ni kwamba, mimi huyo bwana wake sikumtaka na wala sijawahi kutoka naye na kama ningemtaka basi mimi ningeanza kuwa naye kabla yake.

“Ukweli ni kwamba nilikuwa karibu sana na Rammy Galis kwa sababu ya kazi na mpaka sasa tumefanya kazi nyingi ambazo zimetufanya tuwe  karibu.

“Wadau wajue kuwa, sasa mimi na Masogange ni mashosti wa kupika na kupakua. Hatuna bifu tena, mambo yanakwenda. Tena kwa taarifa tu ni kwamba, katika mamodo wanaonisapoti zaidi, Agnes ni zaidi ya wote,” anasema Kidoa.

KUMTEMA MPENZI WAKE BAADA YA KUWA STAA VIPI?

Yapo madai kuwa baada ya kuwa staa alimbwaga aliyekuwa mpenzi wake anayejulikana kwa jina moja la Jeff, hilo nalo limekaaje? Kidoa anafafanua:

“Ni kweli niliachana na Jeff lakini siyo kweli kwamba eti nilimtema baada ya kuwa maarufu, ipo sababu ya kuachana. Sababu yenyewe si nyingine bali alikuwa hajiamini.

“Mapenzi ya kila siku kugombana mimi nilikuwa siyahitaji. Nilimpenda sana Jeff na siyo siri alichangia sana mafanikio yangu, ila ilinibidi niachane naye kwa sababu hajiamini na hajielewi.

“Hilo ni tatizo kubwa sana kwenye mapenzi nikaona ni bora kila mtu achukue ustaarabu. Unajua Jeff, yeye kama mwanaume alitakiwa kujiamini, siyo kuwa na wivu uliopitiliza kama alivyokuwa akifanya,” anasema.

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here