27.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, February 8, 2023

Contact us: [email protected]

KICHUYA USIBADILI GIA ANGANI UTAPOTEA

NA ADAM MKWEPU-DAR ES SALAAM


MWAKA 2015 mratibu wa maendeleo ya soka la vijana nchini, Kim Poulsen, akiwa kocha mkuu wa timu ya Silkeborg IF inayoshiriki Ligi Kuu ya soka nchini Denmark, aliwahi kusema kwamba wachezaji wa Tanzania hawajitambui.

Poulsen alisema kwamba, licha ya Tanzania kubarikiwa wachezaji wenye vipaji vya hali ya juu, lakini tatizo la wachezaji hao wamekosa haiba, tabia, mitazamo na mikakati ya mbele zaidi kitu ambacho kinawanyima nafasi ya kusonga mbele na kucheza soka katika nchi za Ulaya

Kocha huyo aliwataja wachezaji wawili waliokuwa wakicheza soka katika timu ya TP Mazembe ya Kidemokrasia ya Congo, Thomas Ulimwengu na Mbwana  Samatta kuwa ndio waliokuwa na  malengo ya kweli katika kuendeleza vipaji vyao na kupata nafasi zaidi za  kucheza soka barani Ulaya.

Kwa sasa Samatta anacheza barani Ulaya katika timu ya KRC Genk inayoshiriki Ligi Kuu nchini Ubelgiji, wakati Ulimwengu akikipiga AFC Eskilstuna ya Sweden.

Maneno ya Poulsen huenda yakachukuliwa kama eneo la kujifunza kwa baadhi ya wachezaji chipukizi, ambao wanaendelea kuibuka kila  kukicha nchini huku wakitamani kufika kule ambako kila mchezaji hutamani kufika kwa maendeleo ya soka nchini.

Mbali ya kuwa na vipaji vya wakina Samatta na Ulimwengu, bado tunayo hazina ya kutosha ya kupeleka Ulaya na kwingineko kucheza soka la kulipwa.

Wachezaji kama Muzamiru Yassin, Ibrahim Ajib, Deus Kaseke, Geoffrey Mwashiuya na Shiza Kichuya, wanayo nafasi ya kufanya vizuri katika soka la kulipwa nje ya nchi.

Ni jambo la kujipanga pamoja na muda ili kushuhudia ndoto ya mchezaji kama Kichuya ikifuata nyayo za Samatta ya kucheza soka la kulipwa barani Ulaya.

Kwani hadithi nzuri kwa sasa nchini ni kuhusu kipaji cha kinda huyo kutoka Morogoro, anayecheza timu ya Simba ambayo kwa sasa ndiyo kinara wa Ligi Kuu Tanzania Bara.

Mchezaji huyo aliyejiunga na timu hiyo msimu huu akitokea timu ya Mtibwa Sugar, umaarufu wake umeongezeka zaidi baada ya kuonesha soka safi na kufunga mabao nane katika michezo 10 ya Ligi Kuu Tanzania Bara ambayo Simba imecheza.

Hata hivyo, mchezaji huyo anaweza kuzifikia ndoto hizo iwapo hataweza kulinda na kuheshimu kipaji chake na si vinginevyo kwani wachezaji wengi wa aina yake wamepotea kwa kutojitambua na kutotambua wanachohitaji katika soka.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
208,871FollowersFollow
561,000SubscribersSubscribe

Latest Articles