26.7 C
Dar es Salaam
Thursday, September 21, 2023

Contact us: [email protected]

KICHOCHO KINAWEZA KUHARIBU KIBOFU, FIGO

 

Na HERIETH FAUSTINE

KICHOCHO  (bilharzia) ni ugonjwa ambao minyoo midogo aina ya schistosoma huingia katika mwili wa binadamu kwa njia ya vitundu vya ngozi na kusababisha muwasho mwilini.

Pamoja na binadamu kuonekana kuugua ugonjwa huu, wanyama wafugwao kama ng’ombe, mbuzi na kondoo nao wanaweza kupata kichocho pindi wanapotumia maji yenye vijidudu vya maradhi hayo.

Kichocho husababishwa na mambo mbalimbali ikiwamo kuogelea, kuoga, kunywa maji yasiyo salama, kujisaidia katika vyanzo vya maji, kufanya kazi za kilimo kinachohitaji uingie katika maji bila kuvaa mabuti na gloves.

Dalili za kichocho mara nyingi huanza kuonekana baada ya wiki moja tangu mtu apate maambukizi.

Dalili hizi ni  pamoja na maumivu ya tumbo, matatizo katika mfumo wa fahamu, kuumwa kichwa, uchovu, homa, mishipa kukakamaa, kikohozi kuhara, kuwashwa, matatizo ya ngozi pamoja  kinga ya mwili kupungua.

Dalili nyingine ni kuhara damu, kukojoa mkojo wenye kuchanganyika na damu, kuvimba tumbo, ini na bandama kutanuka au huvimba, kuvimba katika maeneo mbalimbali ya mwili yalioathiriwa kwa kichocho, saratani, kuharibika kwa kibofu, matatizo ya figo na hata kusababisha kifo.

Ili kuepuka na ugonjwa wa kichocho inashauriwa kutokuogelea kakika maji baridi kama ziwani, mtoni, katika madimbwi, chemichemi yenye minyoo au vimelea aina ya schistomiasis inayoweza husababisha kichocho.

Kuacha kujisaidia haja kubwa na ndogo katika vyanzo vya maji, hii ni kwa binadamu na wanyama niliowataja hapo juu, hii ni kwa sababu ikitokea kama mtu au mnyama atajisaidia katika maji na ana maambukizi ya kichocho atasababisha vimelea vya kichocho kuathiri maji na hivyo kuwaambukiza wengine watakao tumia maji hayo.

Kunywa maji safi na  salama, epuka kunywa maji yasiyo salama.

Kuoga maji salama, kuchemsha maji hadi yatokote kisha yapoze au yatie chlorine ndipo uyaoge.

Kuvaa viatu kama mabuti na gloves unapoenda kufanya kazi za shamba hasa kilimo kinachohitaji maji mengi.

Kunywa dawa za kinga za kichocho kwa ushauri wa daktari au ambazo hutolewa na serikali katika kuisaidia jamii.

Ugonjwa huu hutibiwa na dawa maalumu dhidi ya vimelea hivi ambazo hupatikana katika kliniki na hospitali yoyote.

Ni vizuri kupima mara kwa mara unapopata shaka ya kuambukizwa kichocho hasa baada ya kutumia maji yenye vimelea vya kichocho.

Makala hii imeandaliwa kwa msaada wa mtandao.

 

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,690FollowersFollow
574,000SubscribersSubscribe

Latest Articles