24.2 C
Dar es Salaam
Thursday, April 25, 2024

Contact us: [email protected]

‘Kichocho husababisha Ukimwi na ugumba’

img_1372CLARA MATIMO Na MASYENENE DAMIAN  

KICHOCHO cha tumbo hushambulia viungo vya uzazi vya mgonjwa na kusababisha ugumba, saratani ya kizazi na maambukizi ya virusi vya Ukimwi.

Hayo yalielezwa  jana na watafiti kutoka Taasisi ya Taifa ya Utafiti wa Magonjwa ya Binadamu (NIMR) kituo cha Mwanza, Dk. Godfrey Kaatano na Dk. Julius Siza.

Walikuwa  wakizungumza na MTANZANIA juzi kuhusu athari ambazo mgonjwa wa kichocho anaweza kuzipata endapo atachelewa kupata matibabu.

Kwa mujibu wa watafiti hao, kichocho cha tumbo  huenea zaidi katika maeneo ambayo shughuli za uchumi hufanyika katika maji.

Waliyataja maeneo yaliyoathirika zaidi nchini kuwa ni ya ukanda wa Ziwa Victoria ambako aina zote mbili za kichocho cha tumbo na mkojo  hupatikakana  huku  kiwango cha maambukizi kikifika  hadi  asilimia 100 katika baadhi ya maeneo.

Dk.   Siza alisema  mayai ya vijidudu  hivyo yana ncha kali ambazo hutoboa mirija ya uzazi na kuharibu kizazi  kusababisha ugumba kwa mwanamke.

Alisema kwa  mwanaume  husababisha majeraha  ambayo husababisha  vimelea vya Ukimwi kujipenyeza kwa urahisi wakati wa kujamaina.

Dk.  Kaatano, alisema mtoto akiugua   kichocho cha tumbo au kichocho cha mkojo   husababisha madhara ikiwamo mahudhurio mabaya shuleni, kudumaa ubongo, ukuaji hafifu na hata akiwa mkubwa hawezi kuzalisha kwa tija.

“Mkoa wa Mwanza uko katika ukanda wa ziwa Victoria ambako kiwango cha maambukizi ya ugonjwa wa kichocho ni cha juu.

“Katika utafiti wa hivi karibuni uliofanywa na mradi wa SCORE katika shule 150 za mkoa huu,   watoto wa shule wapatao 27,926 wenye umri kati ya miaka 6-12 walipimwa na wastani wa kiwango cha maambukizi kilikuwa asilimia 60,” alisema Dk. Kaatano.

“Katika kujikinga na ugonjwa huu tunahimiza zaidi tiba kinga kwa kutumia dawa aina ya Praziquantel na Albendazole na chanjo kwa watoto na wanafunzi kwa sababu ndiyo waathirika wakubwa.

“Lakini tiba hiyo haizuii maambukizi ya kichocho, elimu ya afya, matumizi ya maji safi na salama, matumizi sahihi ya vyoo na kudhibiti konokono ni muhimu,” alisema Dk. Kaatano.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles