28.3 C
Dar es Salaam
Monday, July 22, 2024

Contact us: [email protected]

KICHANGA CHATUPWA PORINI WILAYANI NKASI

Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando.
Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando.

Na Ibrahim Yassin, Nkasi

MTOTO mchanga wa siku moja amekutwa porini akiwa ametupwa na mama yake mzazi katika pori la Chonga Kata ya Myula wilayani Nkasi mkoani Rukwa.

Taarifa iliyotolewa jana na Kamanda wa Polisi mkoani Rukwa, George Kyando ni kuwa mtoto huyo alikutwa katika pori hilo akiwa ametelekezwa na mama yake mzazi muda mfupi tu baada ya kujifungua na kutoweka kusikojulikana hadi sasa.

Alisema mtoto huyo aliokotwa na raia mwema aliyefahamika kwa jina la Flora Lufungulo majira ya saa tisa alasiri akiwa ametokea shambani na ndipo aliposikia sauti ya mtoto mchanga akiwa amehifadhiwa vizuri, huku mama yake akiwa haonekani na ndipo alipotoa taarifa kwenye ofisi ya Serikali ya Kijiji cha Chonga.

Amedai kuwa baada ya taarifa hizo Serikali ya kijiji kwa kushirikiana na wananchi wote katika kijiji hicho walimchukua mtoto huyo na kumpeleka katika kituo kidogo cha polisi Kipande na alipelekwa katika kituo cha afya Kilangala na baada uchunguzi wa kiafya mtoto huyo alikabidhiwa kwenye kituo cha kulelea watoto yatima cha Mission cha Kilangala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
589,000SubscribersSubscribe

Latest Articles