25.1 C
Dar es Salaam
Tuesday, December 10, 2024

Contact us: [email protected]

Kibatala kukata rufaa, aipinga Mahakama Kuu

Bunge
Bunge

Na Kulwa Mzee, Dar es Salaam

WAKILI Peter Kibataka anatarajia kukata rufaa kupinga uamuzi wa Mahakama Kuu kusema kwamba haina mamlaka ya kuingilia marekebisho yanatayofanywa na Bunge Maalum la Katiba katika rasimu.

Kibatala alidai hayo kupitia taarifa yake aliyoitoa jana kupitia mtandao wa kijamii wa facebook ambapo alidai anatarajia kukatia rufaa sehemu ya uamuzi wa mahakama hiyo inayosema kwamba pamoja na kwamba Bunge Maalumu la Katiba lina mipaka na linatakiwa kutekeleza mamlaka yake kupitia Rasimu na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba, yenyewe haina mamlaka ya kusema chochote katika marekebisho yatakayofanywa.

Alidai amefikia hatua hiyo baada ya kujadilina na mteja wake Saed Kubenea kasha kukubaliana hayo.

“Tutakatia rufaa katika Mahakama ya Rufani Tanzania sehemu ya uamuzi wa Mahakama Kuu katika kipengele cha Mahakama kusema kwamba pamoja na kwamba BMK lina mipaka na linatakiwa kutekeleza mamlaka yake kupitia  Rasimu na kifungu cha 9 (2) cha Sheria ya M.y.K, yenyewe mahakama haina mamlaka ya kusema nature na extent ya ammendments na improvements za rasimu.

“Tutakatia rufaa pia kwamba baada ya kusema BMK linaweza ku-ammend na ku-improve rasimu, mahakama ilitakiwa kusema kwamba ammendments na improvements ni tofauti na kutoa kabisa vifungu kadhaa.

“Jumatatu (leo) au Jumanne tutawasilisha kusudio la kukata rufaa Mahakama ya Rufaa wakati tukisubiri Oktoba 7 kusomewa Hukumu yote kwa urefu na mahakama ili tuweze kuona sababu za mahakama katika maeneo kama BMK kukusanya maoni,”alidai.

Alidai wataangalia pia uwezekano wa kufungua shauri chini ya hati ya haraka katika eneo fulani la mchakato.

“Tunaishukuru Mahakama Kuu kwa kile ilichofanya kwa uwezo wake na imechangia sana maendeleo ya Sheria na ya Mchakato mzima. Ila bado tuna kiu katika maeneo tuliyoainisha, tunaona rufaa ni muhimu.

“Kwa nini tunakata rufaa wakati BMK linaelekea mwisho? Mchakato hauishi mpaka kumalizika kura ya maoni,”alidai.

Mwishoni mwa wiki Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam ilisema Bunge Maalumu la Katiba lina mamlaka ya kufanya marekebisho katika Rasimu ya Katiba na si mabadiliko.

Uamuzi huo ulitolewa na jopo la majaji watatu linaloongozwa na Jaji Augustino Mwarija, Aloysis Mujulizi na Jaji Dk. Fauz Twaib.

Mwandishi Saed Kubenea kupitia Wakili wake Kibatala, alifungua kesi dhidi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), akiiomba mahakama hiyo itoe tafsiri sahihi ya Mamlaka  ya Bunge la Katiba, kwa kuzingatia   kifungu cha 25 (1) (2) cha Sheria ya  Mabadiliko ya Katiba na Namba 83  ya mwaka  2011.

Pia anaiomba mahakama itamke kama Bunge hilo lina mamlaka ya kubadilisha maudhui ya Rasimu ya Katiba iliyowasilishwa na Tume ya Mabadiliko ya Katiba na kwa kiwango gani.

Jaji Mwarija akisoma uamuzi huo alisema kutokana na hoja zilizowasilishwa na umuhimu wa suala lenyewe mahakama imeona kuna utata katika tafsiri za Sheria ya Mabadiliko ya Katiba.

“Tafsiri ya kifungu cha 25 (1) (2) cha Sheria ya Mabadiliko ya Katiba namba 83  ya mwaka  201ina utata kwani inatoa maana tofauti katika lugha ya Kiingereza na maana tofauti katika lugha ya Kiswahili.

“Mahakama imeangalia na kupitia sheria, inaona kwamba Bunge Maalum la Katiba lina mamlaka ya kufanya marekebisho ya Rasimu ya Katiba na si kufanya mabadiliko,”alisema Jaji Mwarija.

Alisema pia Mahakama Kuu haina mamlaka ya kuingilia marekebisho yanayofanywa au yatakayofanywa na Bunge Maalum la Katiba kwa sababu hayo ni masuala ya kisiasa na si masuala ya kisheria.

- Advertisement -
Previous article
Next article

Related Articles

1 COMMENT

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
592,000SubscribersSubscribe

Latest Articles