24.2 C
Dar es Salaam
Wednesday, May 31, 2023

Contact us: [email protected]

KIBANO KIPYA MALORI YA MIZIGO KUANZA LEO

Na ANDREW MSECHU

-DAR ES SALAAM

WASAFIRISHAJI mizigo kwa malori katika nchi za Afrika Mashariki wanaotumia barabara za Tanzania wataanza kubanwa kuzingatia matumizi bora ya barabara, kufuatia sheria mpya inayotarajiwa kuanza kutumia leo.

Kuanza kutumika kwa sheria hiyo kulitangazwa rasmi jana na Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kupitia kwa Katibu Mkuu (Ujenzi), Mhandishi Joseph Nyamhanga, ambaye aliwataka wadau wote kuisoma sheria hiyo ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki na kanuni zake.

“Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano inapenda kuwataarifu wasafirishaji na umma kwa ujumla kuwa Sheria ya Udhibiti wa Uzito wa Magari ya Jumuiya ya Afrika Mashariki (EAC Vehicle Load Control Act, 2016) na Kanuni zake za mwaka 2017 itaanza kutumika rasmi nchini Tanzania kuanzi Januari 1, 2019,” ilieleza taarifa hiyo iliyotolewa na Nyamhanga jana.

Alisema tayari tangazo la sheria hiyo lilishachapishwa kwenye Gazeti la Jumuiya ya Afrika Mashariki, yaani EAC Gazette-Legal Notes No. EAC/94/2016 la Novemba 18, 2016 na kanuni zake kutungwa mwaka 2017.

Alisema wizara inatoa wito kwa wasafirishaji wote kuitafuta katika tovuti ya wizara (www.mwtc.go.tz) ili kuepuka adhabu zinazoweza kutolewa kwa kukiuka sheria hiyo.

Nyamhanga alisisitiza kuwa wasafirishaji wote nchini wanatakiwa …

Kwa habari zaidi jipatie nakala yako ya gazeti la MTANZANIA.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,208FollowersFollow
567,000SubscribersSubscribe

Latest Articles