22.8 C
Dar es Salaam
Saturday, June 3, 2023

Contact us: [email protected]

Kibaga FC yaichapa Ulongoni A 1-0 bonanza la TPDC

Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam

Timu ya Kibaga FC iliyopo Kinyerezi Dar es Salaam, imeibuka mshindi katika Bonanza la ujirani mwema lililoandaliwa na Shirila la Maendeleo ya Petroli (TPDC) mara baada ya kuichapa bao 1-0 timu ya kata ya Ulongoni A iliyopo Gongolamboto.

Akikabidhi zawadi kwa timu ya Kibaga mwishoni mwa wiki Meneja Mawasiliano wa TPDC, Marie Msellemu, amesema lengo la bonanza hilo lililoshirikisha timu mbili ni kukuza ushirikiano na ujirani mwema baina ya kata hizo ambazo zimepitiwa na bomba la gesi asilia kutoka Mtwara hadi Dar es Salaam.

‚ÄúTimu ya Kibaga ndio washindi wa mchezo huu, TPDC tunawazawadia mbuzi, jezi, mipira miwili na fedha Sh 100,000 huku timu ya Ulongoni nayo tutaipatia jezi, mipira miwili na Sh 100, 000, aidha, TODC inatumia fursa hii katika kutoa elimu ya gesi asilia kwa wananchi wanaopitiwa na mradi huo,”amesema Marie.

Wenyeviti wa Mitaa ya Ulongoni A, Abdurahim Munisi na Kibaga, Hashim Gulana walishukuru TPDC kwa kuandaa bonanza hilo huku wakieleza kuwa wamejipanga kushirikisha timu nyingi zaidi.

Waliishukuru TPDC kwa kujali vipaji vya vijana huku wakieleza kuwa kila mwezi TPDC wamekuwa wakitoa Sh 300,000 kwa mitaa mitaa yao kwa lengo la kuimarisha ulinzi na usafi katika mitaa hiyo.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
213,270FollowersFollow
568,000SubscribersSubscribe

Latest Articles