Kiba apokewa Kifalme Tabora

0
2581

Mwandishi wetu-Tabora

WAKAZI wa mji wa Tabora, wamejitokeza kwa wingi kumpokea Mfalme wa Bongo Fleva, Ali Kiba aliyefika mkoani hapa kwaajili ya tamasha lake la ‘Alikiba Unforgettable Tour’ linalotarajiwa kufanyika mwishoni mwa wiki katika Uwanja wa Ali Hassani Mwinyi.

Kiba ambaye aliongozana na timu yake, alitua katika Uwanja wa ndege wa Tabora, jana asubuhi na kukuta umati mkubwa wa mashabiki ukimsubiri nje ya uwanja huo huku ukimshangilia kwa kuita ‘Kiba Kiba Kiba’.

Baada ya kutoka uwanjani hapo, Kiba  alikatiza mitaa mbalimbali ya mji wa Tabora akiwa juu ya gari la wazi huku akisindikizwa na shangwe za mashabiki waliokuwa kwenye usafiri wa bodaboda.

Akiwashukuru mashabiki hao, Kiba alisimamisha gari na kusema: “Saluti sana Tabora, nimefurahi kwa mapokezi yenu makubwa, naomba tutulie kidogo, muda wa ‘interview’ umefika, acha nifanye ‘interview’ harafu siku ya tarehe 30 tunaingia uwanjani kufanya shoo.”

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here