MWANAMITINDO maarufu nchini Marekani Khloe Kardashian, ameweka wazi kwamba ameshindwa kumbadilisha mpenzi wake, Lamar Odom, kutokana na tabia yake.
Lamar tangu atoke hospitali ambako alipelekwa baada ya kupoteza fahamu kutokana na utumiaji wa dawa za kulevya na unywaji wa pombe, madaktari walimtaka kuachana na pombe, lakini ameanza kunywa kwa kiasi kikubwa.
“Tangu ametoka hospitali nimejaribu kukaa naye na kumshauri juu ya utumiaji wa dawa za kulevya na pombe, lakini bado matumizi ya pombe yamezidi kuwa makubwa.
“Naweza kusema kwamba nimechoka na siwezi kumsaidia mtu ambaye hayupo tayari kupokea msaada, nadhani nilichokifanya kwake sasa kinatosha hivyo siwezi kumueleza chochote nasubiri matokeo yake,” aliandika Khloe kwenye akaunti yake ya Twitter.