24.5 C
Dar es Salaam
Saturday, April 20, 2024

Contact us: [email protected]

Kheri aeleza CCM itakavyoshinda uchaguzi mkuu

Na TUNU NASSOR -DAR ES SALAAM

CHAMA Cha Mapinduzi (CCM), kimesema kinatarajia kushinda kwa kishindo katika uchaguzi ujao kwa sababu ya mambo zaidi ya nane waliyoyafanya katika jamii na yanaonekana hadharani.

Akizungumza juzi jijini Dar es Salaam, katika mkutano wa vijana wa Chuo Kikuu  cha Dar es Salaam tawi la Abiyani, Mwenyekiti wa Jumuiya ya Vijana wa Chama Cha Mapinduzi (UVCCM), Kheri James alisema katika uchaguzi huo njia ipo nyeupe na wana uhakika wa kuchinja jogoo na kumla mapema bila ya kutoka jasho.

Alisema CCM inajivunia katika ukarabati na ujenzi wa barabara, madaraja, Hospitali, elimu na mengineo hivyo hawana haja ya kujinadi kwakuwa jamii imewaelewa huku akiwabeza wachambuzi wanaotumia fursa mbalimbali kukiponda chama hicho na viongozi wao.

“Inashangaza sana kuna watu kwenye shughuli za chama hawapo, kujenga chama hawapo, kukiimarisha chama hawapo lakini kwenye uchambuzi hawajambo,  hili ni jambo la kijinga sana huwezi kuwa mchambuzi wa kisiasa bila kuwa na misingi au taaluma,”alisema James

Alisema wakiendelea kuwasikiliza wachambuzi hawawezi kufika popote kinachotakiwa ni kila mtu afanye kwa chaguo lake huku akiwaonya kutokubali  uchambuzi kwa watu wasiowajua.

Alisema kwa mwaka huu wamedhamiria kupambana na rushwa hivyo wale watao rushwa watakwenda na maji kwani vitendo hivyo havina msamaha ndani ya chama,

Alisema wamedhamiria kufanya hivyo ili kutoa fursa hata kwa watoto wa maskini kuweza kupata uongozi kupitia CCM.

James alisema ni vema vijana wakatumia nafasi waliyonayo kukijenga chama kwani sifa kubwa ya uteuzi ni kuwaibumtsa wale waliokijenga au mateso kwa chama na nchi pia.

Alisema haitakiwi kuishi kwa kupiga ngoma au elimu kutafuta viongozi bora hivyo ni vema kukijenga chama ili nacho siku moja kukijenga.

Watu wengi wanapotea baada ya chuo kutokana na kukosa marafiki sahihi na ushirikiano na watu walio nje ya chuo alichosoma.

Naye Mwenyekiti wa UVCCM Mkoa wa Dar es Salaam, Mussa Kilakala, alisema wanatarajia kushinda majimbo yote 10 katika jiji hilo.

Alisema wamejipanga vilivyo kuanzia ngazi za matawi kuhakikisha wanashinda nafasi zote kwa Dar es Salaam kwa kuwa wana mfumo mzuri .

“Tumekwisha chinja jogoo wote ili kuua vizazi vya vifaranga hivyo tunatarajia kukabidhi majimbo kumi yote ya mkoa wa Dar es Salaam,”alisema Kilakala.

- Advertisement -

Related Articles

LEAVE A REPLY

Please enter your comment!
Please enter your name here

Stay Connected

90,904FansLike
214,997FollowersFollow
586,000SubscribersSubscribe

Latest Articles